1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yachukua hatua.

Mtullya, Abdu Said8 Oktoba 2008

Uingereza yatenga pauni bilioni 50 kuyasaidia mabenki.

https://p.dw.com/p/FWCf
Waziri wa fedha wa Uingereza Alistair Darling.Picha: AP

Masoko muhimu ya hisa yanaendelea kuanguka duniani kote, licha ya hatua kubwa zinazochukuliwa na serikali kadhaa katika juhudi za kuukabili mgogoro wa fedha.Pamoja na hatua hizo ni uamuzi wa serikali ya Uingereza kutangaza mpango wa kutaifisha sehemu ya mabenki makuu ya nchi.

Uingereza imetangaza mpango wa kutenga pauni bilioni 50 katika juhudi za kuutia nguvu mfumo wa benki wa nchi hiyo.Waziri wa fedha wa Uingereza Alistair Darling amesema hayoa katika tamko na kueleza kuwa hatua hiyo itakuwa na maana ya kutaifisha sehemu ya mabenki makuu ya nchi.Licha ya hatua hiyo iliyochukuliwa na nchi inayoshikilia nafasi ya tatu katika nguvu za uchumi barani Ulaya, masoko muhimu ya hisa yameendelea kushuka.

Katika tamko lake waziri Darling pia amefahamisha kuwa Benki Kuu,Bank of England itatenga pauni bilioni 200 ili kuyawezesha mabenki kuchukua mikopo.

Waziri Darling ameeleza kuwa hatua zinazochukuliwa zinalenga shabaha ya kuleta utengemavu katika mfumo wa fedha nchini Uingreza.Waziri huyo amesema anatumai hatua zilizochukuliwa zitasaidia katika kurejesha imani,kufufua na kuchapua uchumi wa Uingereza.

Akizungumza juu ya hatua hizo waziri mkuu wa Uingereza G.Brown amesema lengo ni kuimarisha mfumo wa mebenki nchini Uingereza. Na kwa mara ya kwanza waziri mkuu Brown amezungumzia juu ya ulazama wa kuwapo mpango wa pamoja kwa nchi zote za Ulaya juu ya kuukabili mgogoro wa fedha.Waziri Mkuu Brown amesema anafanya mashauriano na viongozi wengine juu ya jinsi ya kupitisha mpango huo.Lakini licha ya hatua hizo soko la hisa la Uingereza FTSE lilianguka kwa asilimia 5.