1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Faida za simu ya Smartphone

15 Agosti 2016

Miaka 20 tangu simu ya "Smartphone" ilipoingia kwenye soko la mawasiliano, na kuleta mapinduzi ya kimawasiliano barani Afrika, ambako sasa inatumika kama chombo cha kupashana habari za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

https://p.dw.com/p/1JiOw
Pokemon Go in AfrikaPicha: Getty Images/S.Heunis

Waafrika wasiopungua milioni 80 walikuwa na simu ya mkononi mnamo mwaka 1999. Mwaka 2008 idadi hiyo iliongezeka na kufikia watu 500 milioni - hiyo ikiwa sawa na asilimia 60 ya wakaazi jumla wa bara la Afrika. Mnamo mwaka 2015, kwa mujibu wa kamapuni inayotengeneza simu za mkononi chapa Ericsson, kulikuwa na mikataba takriban bilioni moja ya simu za mkononi kote barani Afrika. Wataalam wanakadiria kuna simu bilioni mbili za mkononi zinazokutikana barani Afrika na katika eneo la Mashariki ya Kati. Nusu ya simu hizo ni aina ya Smartphones, anasema mkurugenzi wa kanda ya kusini mwa Afrika wa shirika la kimataifa la Data Corpotration - IDC, Martin Walker:"Kuendelea kupungua thamani kwa teknolojia ya Smartphone na kuzidi kuboreka kwa mawasiliano kupitia mtandao pamoja pia na kuongezeka nguvu za mtandao hadi kufikia 3G na 4G -yote hayo yamechangia kuifanya Smarthphone izidi kuwavutia watu. Wakati huo huo, ufundi wa kutengeneza Smarthphone kuambatana na mahitaji ya bara la Afrika umeongezeka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita."

Smartphone kama chombo cha kuitisha maandamano

Hadi mwaka 2017, idadi ya Waafrika wanmaotumia simu za mkononi aina ya Smartphone inatarajiwa kuongezeka mara dufu. Kwa mujibu wa taasisi ya ushauri wa masuala ya kiuchumi - Deloitte, hadi ifikapo mwakani barani Afrika kutakuwa na simu zaidi ya milioni 350 za mkononi zenye mtandao wa intaneti. Hiyo ni fursa kubwa kwa wenye kutengeneza programu za kibiashara kupitia simu za mkononi na kwa mahitaji ya Waafrika. Hata hivyo, simu za mkononi hazitumiwi pekee kwaajili ya masuala ya kiuchumi. Kutokana na kuwepo simu zaidi za mkononi barani Afrika, watu wanazitumia simu hizo za tekonolojia ya kimamboleo pia kuitisha maandamano ya kisiasa dhidi ya tawala zao.

Infografik Smartphones vs Mobiltelefon in Afrika deutsch
Ramani ya jinsi Smarphone ilivyoenea Afrika na Mashariki ya kati

Kwa mujibu wa Professor Marco Manacorda wa Chuo Kikuu cha Queen Mary cha mjini London, simu za mkononi zinatumika pia kueneza ripoti kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi kwa haraka zaidi. Anasema kwa kupashana habari watu wanafanikiwa kujuana pia.

Serikali hazipakati mikono

Prof. Manacorda anahisi serikali pia zinajifunza jinsi ya kuitumia teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kama chombo cha upelelezi. Na mara nyingi wanazifunga njia hizo za mawasiliano.

Nokia Communicator 9000, das erste Smartphone der Welt, 1996
Smartphone ya kwanza kabisa dunianiPicha: dpa/Nokia

Mwandishi: Krinninger,Theresa/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Khelef