1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 25 ya mahakama ya uhalifu kwajili ya Rwanda

Sekione Kitojo
7 Novemba 2019

Miaka 25 imetimia baada ya kuundwa mahakama ya Rwanda kuwahukumu wale waliohusika katika mauaji ya kimbari nchini humo mwaka  1994. Wakati mauaji hayo yakiendelea jamii ya kimataifa ilishindwa kuchukua hatua.

https://p.dw.com/p/3SbVO
Ruanda Internationaler Gerichtshof für den Völkermord
Picha: picture-alliance/dpa/L. Lee Beck

((Lakini  baadaye  iliundwa  mahakama  ya  kimataifa  ya  kuwahukumu wahalifu walioshiriki  katika  mauaji  hayo  nchini Rwanda. Inawezekana  mahakama hii  ya uhalifu ikarejeshwa tena baada  ya  kufungwa? Jibu  ni la  mkanganyiko. 

Niederlassung des internationalen Straftgerichtshofs für Ruanda ICTR in Kigali
makao makuu ya mahakama ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda mjini Arusha ICTRPicha: DW/A. Le Touzé

Ruanda  mwaka  1994, redio ya  wenye misimamo  mikali  ya kisiasa  wanatoa  wito  wa  mauaji, na Wahutu wenye misimamo mikali  wanawauwa  bila  huruma  raia  wa  jamii  ya  wachache  ya Watutsi  pamoja  na  Wahutu  wenye  msimamo  wa  kati, na  miili yao  ikatupwa  mtoni. Katika  muda  wa  chini  ya  siku 100 kwa makadirio  ya  Umoja  wa  mataifa  kiasi ya  watu 800,000  na milioni  moja  walisakwa  na  kuuwawa. Dunia  ikiwa  inatazama  tu. katika  uhalifu  huu , ambao  ni  mbaya  kabisa  katika  historia  ya binadamu , jamii  ya  kimataifa  ilitaka  kutoa onyo. Kwamba hatimaye  inataka  kujadili  na kuthibitisha kwamba  sheria  za kimataifa  dhidi  ya  uhalifu  sio  maneno  matupu , badala  yake inawezekana.
 

Siku 100 nyingine baadaye , tarehe 8 Novemba  mwaka  1994, baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa  liliidhinisha mahakama ya  muda  kwa  ajili  ya  kuwahukumu  wahalifu. Mwanzoni  mwa mwaka  1995  mahakama ya  kimataifa  ya  uhalifu  kwa  ajili  ya Rwanda  ICTR ilianza  kazi  katika  mji  wa  kaskazini  mwa  Tanzania wa  Arusha. Pamoja  na  kufanyakazi  kwa  kile  kinachojulikana kama  mahakama  za  kienyeji  za  Gachacha, wahusika  wakuu walipelekwa  mjini  Arusha  kuwajibishwa. Ni jaribio  la  sheria  na mahakama  ya  kimataifa.
 

Fatou Bensouda
Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague Fatou BensoudaPicha: AFP/Getty Images

Mahakama yafika mwisho

Baada  ya  miaka  21  mahakama  ya  kimataifa  ya  ICTR  ilifikisha mwisho  shughuli  zake  mwanzoni  mwa  mwaka  2016. Boubacar Diallo  hadi  hii  leo  akiwa  mwendesha  mashitaka  mkuu  wa  ICTR , alikuwa  akipata  shida  kutoa tathimini  chanya: "Kwa kiasi kikubwa tumefanyia kazi  masuala  mengi" anasema  katika mahojiano  na  DW. mahakama  ya  rwanda  iliwafikisha mahakamani , wakuu  wa  jeshi, wanasiasa , waandishi  habari  na pia  wakuu wa serikali , ambao  walihusika  katika  mauaji  ya kimbari. Zaidi  ya  hayo  mahakama  ya  ICTR imetayarisha  sehemu kubwa  ya  sheria zake , ambazo  leo  zinatumika  kama mifano katika  mahakama  nyingine  duniani  kote. " Mahakama  hii  inaweza kwa  hiyo  kuwa  muhimu  katika  mapambano  dhidi  ya  ukosefu wa kupatikana  haki  katika  dunia  yetu", amesema  Diallo.

Tanzania Rwanda Genocide Verdict
Mmoja kati ya washitakiwa katika mahakama ya ICTR Theoneste Bagosora Picha: AP

Mwaka  1998 mahakama  ya  rwanda  kama  mahakama  ya  kwanza ya  kimataifa  ilitoa  hukumu  mhalifu  wa  kwanza  kutokana  na mauaji  ya  kimbari. Karibu  nne  ya  tano  ya  wahalifu waliohusika na  mauaji  hayo  ya  kimbari  mwaka  1994  katika mwaka  uliofuata walikamatwa  na  kufikishwa  mahakamani.  Mahakama  ya  ICTR iliwafikisha  mbele  ya  sheria  washitakiwa 93. 61 walipatikana  na makosa , 14 waliachiliwa  huru. Wengi  wa  wachunguzi wanakubaliana , kwamba  kwa  kiasi  kikubwa  na  kwa  jumla mahakama  ya  ICTR imetimiza  wajibu  wake.
 

Geraldine Mattioli-Zeltner  kutoka  shirika  la  kutetea  haki  za binadamu  la  Human Rights watch  anathibitisha  kuwa , ICTR imekuwa  ni  sehemu  kubwa  ya  ujenzi  wa  taasisi ya  kimataifa  ya kufuatilia  wahalifu  dhidi  ya  ubinadamu. Mahakama  ya  uhalifu  ya Rwanda  ni  jiwe  la  msingi  ka a  ujenzi wa  mahakama  ya kimataifa  mjini  The Hague. Washitakiwa  wapya  hawatapelekwa tena mjini  ARUSHA.