1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 50 tangu ukandamizaji wa vuguvugu la mageuzi Prague

Sekione Kitojo
21 Agosti 2018

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Czech Andrej Babis alizomewa  wakati akitoa hotuba katika kumbukumbu ya miaka  50 ya uvamizi  ulioongozwa na uliokuwa Umoja wa Kisovieti kuivamia iliyokuwa Czechoslovakia ya zamani.

https://p.dw.com/p/33V4r
Prager Frühling - Einmarsch
Vifaru vya majeshi ya mkataba wa Warsaw vikiingia mjini Prague Picha: picture-alliance/akg-images

Miaka  50  iliyopita  vifaru  vya  iliyokuwa  Umoja  wa Kisovieti  viliingia  mjini  Prague  kuzima mageuzi ya kidemokrasia ya  serikali  ya  kikomunist  ya  Czechoslovakia, na  kuzusha umwagaji  damu katika hatua  ya  kuikalia  nchi  hiyo  ambapo somo lililopatikana Waczech wengi wanalihofia limesahaulika.

1968 - Ende des Prager Frühlings
Majeshi ya mkataba wa Warsaw yalivyoingia mjini Prague na kuzima vuguvugu la mageuzi katika Czechoslovakia ya zamani Picha: Arte

Kumbukumbu  hiyo  ikifanyika  kwa  sherehe, maonesho na  filamu juu  ya  vuguvugu  la   mapinduzi  ya  Prague  pamoja  na ukandamizaji  wake  wa kikatili  ambao  ulianza  Agosti 21, 1968, inakuja katika  wakati  kuna ushawishi  unaorejea  tena  katika chama  ambacho  kwa  muda  mrefu  kiliwekwa  kando  cha kikomunist cha  Czech  katika  siasa  za  taifa  hilo.

Babis, ambaye  aliwahi  kuwa  mwanachama  wa  chama  cha Kikomunist  cha  Czechoslovakia, alikuwa  akizungumza  katika kumbukumbu  hiyo  wakati  maneno  yake  yalimezwa  na  kelele  za kumzomea  na  kulele  za "aibu"  kutoka  kwa  kundi  la  watu waliokuwa  wakisikiliza  hotuba  hiyo. Babis alisema.

Tschechien Andrej Babis
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Czech Andrej BabisPicha: Reuters/D. Cerny

"Watu hawakutaka  tena  udikteta wa  aina  ya  Kisovieti. Walitaka  tu  kuishi  maisha  ya  kawaida, ya jamii  huru. Uvamizi wa  majeshi  ya  mkataba  wa  warsaw yalizuwia  hatua  za mageuzi  na ubinafsishaji."

Babis  ambaye  ni  muasisi  wa  chama  cha  ANO , amekuwa  waziri mkuu mwaka jana. Amekabiliana  na  ukosoaji  mkubwa  unaohusiana na  chama  chake  cha  zamani cha  kikomunist.  Akizungumza  katika kumbukumbu  hiyo katika  jengo  la  redio  ya  Czech, eneo  ambalo machafuko  makubwa  yalitokea  wakati  wa  uvamizi  wa  mwaka 1968, Babis alitoa  heshima  zake kwa  wale  waliofariki.

Ukandamizaji wa  nguvu

Miezi michache ya kuchukua madaraka  kama kiongozi wa chama cha kikomonisti cha iliokuwa Czechoslovakia mwanzoni mwa mwaka 1968, Alexander Dubcek alifuta ukaguzi wa kisiasa, na kujaribu kuleta mageuzi ya kiuchumi. Vikosi vya kisovieti yaani Urusi ya zamani, Poland, Hungary na Bulgaria viliingia katika mji mkuu wa Czechoslovakia -Prague wakati wa usiku wa Agosti 20-21 mwaka huo  na kufanya ukandamizaji wa kikatili katika kile walichokiona ni kitisho kikubwa kwa ushawishi wa kisiasa  wa  Urusi.  Wanahistoria wanasema raia 137 waliuawa katika ukandamizaji huo kati ya Agosti na Desemba mwaka 1968.

Josip Broz Tito
wakati wa mbinyo mkubwa kutoka Urusi kutaka kusitisha mageuzi ya kisiasa nchini Czechoslovakia , rais Josip Tito wa Yugoslavia alitembea nchini humo na kuunga mkono mageuziPicha: picture-alliance/CTK Photo/J. Rublic

Wakati huo huo kukumbuka tukio hilo  la miaka 50 iliopita, Mamia ya waandamanji walikusanyika nje ya ubalozi wa Urusi mjini Prague jana jioni  ili kupinga  hatua ya Urusi wanaoiona kuwa ya ukandamizaji mwengine baada ya kulitwaa eneo la  Crimea kutoka nchi jirani ya Ukraine mwaka 2014.

Wanasiasa  maarufu  wa  Umoja  wa  Ulaya  wamesema kumbukumbu  hiyo  pia  inaeleza haja  ya  kulinda  uhuru  na demokrasi  leo  katika  bara  ambalo  linakabiliwa  na  wimbi  jipya  la tawala za  ukandamizaji  katika  Ulaya  mashariki, pamoja  na  Urusi ambayo inajaribu  kuweka  ushawishi  wake  katika  maeneo yake ya zamani.

Tscheschien Prag - Andrej Babis bei Gedenkfeier der Niederschlagung vom Prager Frühling 1968
Maandamano dhidi ya chama cha ANO cha waziri mkuu Andrej BabisPicha: Imago/CTK Photo/R. Vondrous

"Agosti 21 , 1968  ilikuwa sawa na  konde lililovurumushwa  usoni," alisema  Vladimir Hanzel, akikumbuka  ghasia  mpya  zilizotokea wakati  huo  ambapo  wanajeshi 200,000  wa  kile  kilichofahamika kama  mkataba  wa  Warsaw , wengi  wao  kutoka  iliyokuwa Umoja wa  Kisovieti  lakini  pia  Poland, Hungary na Bulgaria, waliingia katika  nchi  hiyo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Mohammed  Abdul Rahman