1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIAMI:Manuel Noriega kurudishwa Ufaransa mwezi ujao

29 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUv

Dikteta wa zamani nchini Panama Manuel Noriega atarudishwa Ufaransa mwezi ujao baada ya kukamilisha kifungo cha miaka 17 anachoendelea kutumikia katika jela ya Marekani baada ya kuhukumiwa kwa kosa la usafirishaji wa mihadarati.

Uamuzi wa kurudishwa nchini Ufaransa kwa Noriega uliidhinishwa na Jaji William baada ya mawakili wa serikali ya Marekani kupendekeza Noriega mwenye umri wa miaka 73 apelekwe Ufaransa ambako anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela kwa kukutikana na hatia ya kuhusika katika wizi wa fedha.Wakati huohuo Panama imesema itafanya kila iwezalo kumrudisha Noriega nchini humo ingawa upinzani nchini humo unapinga hatua hiyo.Noriega alikuwa mshirika wa karibu wa Marekani wakati wa vita baridi na alikuwa jasusi wa shirika la CIA kwa miaka mingi.Lakini urafiki wake na Marekani ulikatika aliposhtakiwa kwa kuhusika katika usafirishaji wa mihadarati.