1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 24 ya wamahamiaji yapatikana Libya

Sekione Kitojo
28 Juni 2017

Wafanyakazi wa kujitolea wa Shirika la Hilali Nyekundu wamepata miili ya watu 24 wahamiaji iliyosukumwa na maji hadi ufukweni mashariki mwa Tripoli, huku uokoaji ukiendelea katika Bahari ya Mediterania. 

https://p.dw.com/p/2fXxg
Spanien Boot der Küstenwache im Hafen von Tarifa
Picha: Getty Images/AFP/M. Moreno

Wakaazi katika  wilaya  ya  Tajoura  wamesema  miili  hiyo  ilöianza  kusukumwa hadi  ufukweni  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita. MiilI kadhaa  imekuwa  imeharibika  na  kuliwa  na  mbwa , kwa  mujibu  wa  afisa  wa  kikosi  cha  ulinzi  wa  pwani. 

Idadi  hiyo ilitarajiwa  kupanda  wakati  maboti  mabovu  yanayotumika  kuwasafirisha  wahamiaji  hadi  katika  maeneo  ya  kimataifa ya  bahari  kwa  kuwa  kwa  kawaida  hubeba   zaidi  ya  watu  100. 

Wahamiaji  watatu  walifariki  katika  bahari  ya  Mediterania  usiku  wa  Jumatatu , shirika  la  kutoa  misaada  la  Ujerumani  lilisema, wakati operesheni  ya uokozi ikiongozwa  na  Italia ambapo maelfu  zaidi  waliokolewa.