1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Umoja wa Ulaya wataka mapigano kusitishwa Gaza

Lilian Mtono
27 Oktoba 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuachwa njia salama kwa msaada wa kiutu. Baada ya majadiliano ya saa kadhaa ya Baraza la Ulaya.

https://p.dw.com/p/4Y5Gd
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanahimiza ufikishwaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza na kusitishwa mapigano
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanahimiza ufikishwaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza na kusitishwa mapiganoPicha: Dario Pignatelli/European Union

Wakuu hao wa Ulaya, wamesema Umoja wa Ulaya utashirikiana na washirika katika Kanda ya Mashariki ya Kati kuwalinda raia, na kuwafikishia msaada wa chakula, maji, dawa, mafuta na makaazi, wakihakikisha kuwa msaada huo ''hauwanufaishi magaidi.'' 

Wakati huo huo, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura kuanzia jana kujadili vita vya Israel na Hamas.

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour alilitaka baraza hilo kutambua mateso makubwa yanayowafika Wapalestina katika vita hivyo alivyosema baadhi ya nchi wanachama umoja huo wanaviunga mkono.

Naye balozi wa Israel Gilad Erdan amejibu kuwa nchi yake haipigani vita na Wapalestina, bali "kundi la kigaidi la Hamas."