1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miji mikubwa Iran yakumbwa na maandamano

Sekione Kitojo
17 Novemba 2019

Waandamanaji waliokasirishwa na kupandia kwa bei ya mafuta Iran kwa asilimia 50 wamefunga barabara katika miji mikubwa na  walipambana mara kwa mara na polisi jana Jumamosi baada ya kupambana na polisi.

https://p.dw.com/p/3TAqq
Iran Weiter Unruhen - Kaum noch Zugang zum Internet
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Khahi

Katika  ghasia hizo inaripotiwa kuwa  kiasi  mtu  mmoja ameripotiwa kuuwawa.

Maandamano  hayo yameweka  mbinyo  mpya  dhidi  ya  serikali  ya Iran wakati  ikihangaika  kuondokana  na  vikwazo vya  Marekani vinavyoikaba  nchi  hiyo  baada  ya  rais Donald Trump  wa Marekani kuitoa  nchi  hiyo  kutoka  katika  makubaliano  ya kinyuklia  kati ya  Iran  na  mataifa  yenye  nguvu duniani.

Iran Weiter Unruhen - Kaum noch Zugang zum Internet
Waandamanaji wamejikusanya huku pikipiki ikichomwa motoPicha: AFP

Katika  maandamano  ambayo  kwa  kiasi  kikubwa  yalikuwa  ya amani ,  maandamano yaligeuka  kuwa  ya  ghasia  katika  maeneo kadhaa, ambapo  vidio  zilizowekwa  katika  mtandao  zilionesha polisi  wakifyatua  mabomu  ya  gesi  ya  kutoa  machozi  na makundi  ya  watu  yakiwasha moto. Wakati  yakiwakilisha  kitisho cha  kisiasa  kwa  rais Hassan Rouhani  kabla  ya  uchaguzi  wa bunge  mwezi Februari, pia  yanaonesha ghadhabu  ilisosambaa kwa  watu  wengi  miongoni  mwa  Wairan  milioni  80 ambao wameshuhudia  hifadhi  yao  ya  fedha  ikiyeyuka kutokana  na ukosefu  wa  ajira na  kuporomoka  kwa  sarafu  ya  taifa  hilo ya rial.

Maandamano  yalifanyika  katika  miji  zaidi  ya  12  katika  muda kufuatia  uamuzi  wa  Rouhani  mapema  siku  ya  Ijumaa  kupunguza ruzuku  katika  mafuta ili  kugharamia  fedha  zitolewazo  kwa  watu masikini  nchini  humo. Mafuta  nchi  humo  bado  yanabaki  kuwa rahisi  duniani, ambapo  bei  mpya  imepanda  hadi  rial 15,000 kwa lita  moja, ikiwa  ni  ongezeko  la  asilimia  50 kutoka  siku  moja kabla. Hii  ni  senti 13  kwa  lita, ama  kiasi  ya  senti 50 kwa  galoni moja. Galoni  ya  mafuta  ya  kawaida  nchini  Marekani ni kiasi  ya dola 2.60, ukilinganisha.

Iran l Proteste gegen höhere Benzinpreise
Magari yamezuwia barabara kuu Picha: picture alliance/AP Photo

Mafuta bado ni  bei ya chini

Lakini  katika  taifa  ambako  wengi wanaendesha  maisha  yao kama  madereva  wa  teksi  ambao  sio rasmi, mafuta  rahisi yanaonekana  kuwa  haki  ya  kuzaliwa. Iran  ni  nchi ya  nne  duniani yenye  hazina  kubwa  ya  mafuta ghafi. Wakati ikitarajiwa  kwa miezi  kadhaa, uamuzi  huo  bado  umewafikia  watu  wengi  bila  ya kutarajia  na  kuzusha  ghafla  maandamano.

Ghasia  zilizuka  siku  ya  Ijumaa  usiku katika  mji  wa  Sirjan, ulioko kilometa 800 kusini  mashariki  mwa  tehran. Shirika  la  habari  la nchi  hiyo IRNA limesema, waandamanaji  walijaribu  kuchoma  moto kituo cha  kuhifadhi  mafuta, lakini  walizuiwa  na  polisi.

Iran l Proteste gegen höhere Benzinpreise
Waandamanaji katika mji wa Khorramshar nchini IranPicha: picture alliance/dpa

Polisi hawakutoa  taarifa  zaidi, lakini  vidio zilizowekwa  mtandaoni nchini  Iran zinaonesha moto katika  kituo  hicho  cha  kuhifadhi mafuta wakati magari ya  polisi yakisikika. Vidio  nyingine  inaonesha kundi  kubwa  la  watu  likipiga  kelele: Rouhani, aibu  kwako ! Ondoka  nchini  peke  yako !"

Mohammad Mahmoudabadi, afisa  wa  wizara  ya  mambo  ya  ndani katika  mji  wa  Sirjan, baadaye  aliimbia  televisheni  ya  taifa  kuwa polisi  na  waandamanaji  walishambuliana  kwa  risasi, na  watu kadhaa  kujeruhiwa. Amesema  mandamanaji  mengi yalikuwa  ya amani, lakini  baadaye  watu  waliojifunika  nyuso  zao wakiwa  na bunduki  na  visu walijiingiza  katika  maandamano  hayo.