1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milio ya risasi imesikika bunge la Uingereza

Yusra Buwayhid
22 Machi 2017

Afisa mmoja wa polisi amechomwa kisu nje ya jengo la bunge la Uingereza, baada ya kuvamiwa na mshambuliaji ambaye baadae alifyatuliwa kwa risasi na polisi huku kukiwa na taarifa za majeruhi katika daraja la Westminster.

https://p.dw.com/p/2Zkj6
Großbritannien London
Picha: Getty Images/J. Taylor

Polisi wa mji mkuu wa London wamesema wanalichukulia tukio la daraja la Wesminster kuwa ni la kigaidi. Watu walioshuhudia shambulio hilo la kwenye daraja wamesema waliona gari likiwavamia watu kadhaa. Huku walioshuhudia tukio la bungeni wakisema kuwa walisikia milio ya risasi. 

Polisi waliojihami kwa silaha wamelizingira eneo hilo la bunge pamoja na daraja la Wesminster, na polisi wamewataka wabunge kubaki ndani ya jengo hilo. David Lidington, ambaye ni kiongozi wa bunge la Uingereza amesema hadi sasa anachoweza kuthibitisha ni kwamba kumetokea shambulio katika bunge hilo.

Aidha imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza yupo salama baada ya kuoneka akiingia ndani ya gari iliyomuondosha katika jengo la bunge.

Mashambulio hayo yametokea katika siku ambayo Ubelgiji inatimiza mwaka mmoja tokea mashambulio kwenye uwanja wa ndege na kituo cha treni mjini Brussels yalioyosababisha vifo vya watu 32.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/ape/rtre/afpe

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman