1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MINSK: Belarusia imepeleka ujumbe Russia kushauriana kuhusu malipo ya gesi

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfC

Belarusia imepeleka ujumbe mjini Moscow kujaribu kutanzua mzozo kuhusu malipo ya gesi inayouziwa na Rusia.

Afisa wa wizara ya nishati wa Belarusia amesema ana imani kwamba mzozo huo utapatiwa ufumbuzi kabla ya mwisho wa mwaka.

Hata hivyo, afisa huyo hakusema endapo serikali yake itayakubali matakwa ya kampuni ya Gazprom iliyoongeza ada hiyo kwa asilimia mia mbili.

Kampuni hiyo imetishia kukatiza huduma yake kwa Belarusia Januari mosi endapo nchi hiyo haitaridhia nyongeza ya bei iliyowekwa.

Nayo Belarusia imetishia kuizuia Russia kupitishia nchini humo gesi inayouzia mataifa ya Ulaya.