1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mipango kwa miji mikuu-Mega Cities.

25 Mei 2009

Umuhimu wa kupanga miji.

https://p.dw.com/p/HxDe

Kila kukicha, watu zaidi wanahamia mijini kutoka mashambani. Miji mikuu iliosheheni wakaazi (Mega Cities), tayari hii leo imegeuka kitisho kwa mazingira yetu. Nchini Pakistan, kwa hivyo, mabingwa wanadai kutungwa kwa fikra mpya katika kupanga miji:

Pakistan ina mabingwa wazuri sana wa mipango ya miji kwa muujibu asemavyo Usman Mustafa wa Taasisi ya Pakistan ya maendeleo ya kiuchumi. Kwa bahati mbaya, mipango hiyo haitekelezwi ipasavyo. Serikali nayo inavutwa huku nya kule baina ya azma zake inazolenga zinazopingana. Ni la kwanza kutenda katika hali kama hiyo? Katika miji mikubwa kabisa kama vile Karachi je, inapasa kuweka kabdo maeneo ya kupanuka kwa mji kama huo ?

Usman Mustafa anaona kuwa miji mikubwa sana kuzidi kuikuza ni kuongoza katika misukosuko na matatizo zaidi. Kwa hivyo, mabadiliko ya fikra katika kupanga miji kunahitajika mno na haraka:

Mji wa Karachi umechaguliwa kuwa mji wa kupigiwa mfano nchini Pakistan. Una vyuo vikuu vingi, maeneo ya viwanda na ya biashara huru. Ukiwa na uwanja wa ndege wa Kimataifa na bandari kubwa ya kisasa inayohudumia hadi 60% ya shehena za mizigo za nchi hii. Kulingana na mfumo wa China ulioipatia maendeleo, Karachi umepangwa kuwa gurudumu la maendeleo ya uchumi ya Pakistan kupitia raslimali za kigeni.

Upande wa pili wa sura hii ni kuchafuka kwa mazingira. Maji ya pwani yake jinsi yalivyochafuka, uvuvi umeathirika. Barabara ambazo katika msimu wa mvua za monsun baadhi yake hujaa maji hadi mita 1, zinafunikwa na jaa. Mitaa ya madongo poromoka wanamoishi masikini inazidi kupita kiasi na kwa kasi mno. Maradhi mengi ya kuambukiza yanatapakaa kutokana na ukosefu wa hali za usafi zinazotokana na matatizo ya miji mikuu, Mega City-inayokaliwa na zaidi ya watu milioni 20.

Usman M ustafa anasema:

"Ikiwa kote kutajengwa vyuo vikuu kama vile Karachi, basi watu wengi watahamia. Viwanda vikiundwa hapa, watu watakimbilia hapo na kutumia nafasi hizo za kazi. Juuu ya hivyo, mimi napinga miji mikuu kupita kiasi, Mega Cities-kwani miji kama hiyo inasababisha matatizo makubwa .Sio tu matatizo ya kiuchumi, bali pia ya kijamii, ya miundo-mbinu na hata ya maji ya kunywa."

Bw. Usman Mustafa ni kiongozi wa Idara ya kutathmini miradi katika Taasisi ya Pakistan juu ya maendeleo ya kiuchumi mjini Islamabad-Taasisi maarufu kabisa inayoongoza katika kupanga mipango kote barani Asia.

Anasema katika miji mikuu kama hiyo, mipango ya miji ni jambo lenye kuwekwa sio usoni kabisa. Miji kama hii inazusha matatizo kote ulimwenguni. Hatua ya maana ni bora kujenga miji mengine midogo-midogo sehemu za mashambani ili kuzuwia kila mmoja kuhamia mjini. Miji hiyo midogo iwe ya kuvutia. Viwanda vijengwe huko na kuwapo mipango ya kuwapatia wakaazi mahitaji yao ya kimsingi. Ikiwa watahudumia mitaa ya madongoporomoka, basi mitaa mengine itachomoza karibu na hapo. Na hivyo, ni shida kwa serikali yoyote kuiendesha na kuongoza.

Serikali ya Pakistan inajaribu kwa hivyo, hata sehemu za mashambani kufikisha ufundi wa ki-mamboleo na nafasi za kazi -kwa muujibu asemavyo Zafar Iqbal Zaidi, mkurugenzi wa Baraza la Pakistan la nishati inayopatikana tena na tena.

Usman Mustafa anatoa nasaha kwa wapangaji-miji: Anasema miji inayotia maanani watu wake wanaotembea kwa mguu, huvutia. Kuwa na usafiri wa umma badala ya ule wa watu binafsi. Nchini Pakistan, wenye magari wana fursa bora kuliko wale wanaosafiri kwa vyombo vya umma.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Josephat Charo