1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yasema haitawazuia kwa sasa wapalestina kutoka Gaza

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cy6n

RAFAH:

Misri imesema haitawazuia waPalestina wa Gaza kuingia na kutoka nchini mwake.Hata hivyo itadhidibiti wale wanaotumia magari na wala sio wanaotumia miguu.Polisi ya Misri ikitumia vifaru imeziba baadhi ya vivuko. Maelefu ya wa Palestina wanaendelea kumiminika katika mpaka wake na Gaza. Baado watu wengi wanaingia na kutoka kupitia mpaka huo baada ya juhudi za Misri za kuufunga kushindwa siku ya Ijumaa. Wapalestina hao wanajilimbikizia bidhaa muhimu kama vile chakula na mahitaji mengine. Hii ni kufuatia uhaba wa vitu hivyo uliyosababishwa na mzingiro wa hivi majuzi wa Isreal. Isreal, kwa upande wake, inasema mzingiro huo ulikuwa na nia ya kujaribu kuzuia uvurumishwaji wa maroketi kutoka Gaza hadi Israel.Hata hivyo imeshutumiwa kwa ,adhabu isiokubalika, kwa watu wote wa Gaza bila kujali watu wasio na hatia.Kiongozi wa Palestina Mahmood Abbas amewaomba wapiganaji wa Hamas kuacha kuivurumishia makombora Israel na wakati huohuo kuilaumu Israel kwa kufunga mipaka yake na Gaza.

Kwa mda huohuo,baado kuna utata katika taarifa kuwa rais wa Misri amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano wa makundi ya kipalestina yanayohasiamiana.Kundi la Hamas ,ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza,linaonekana kukubali mwito huo,lakini wizara ya mashauri ya kigeni ya Misri imeziita taarifa hizo kama sio na ukweli.Hata hivyo mipango imetangazwa ya mkutano kati ya waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas kujadilia mgogoro huo.