1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mitetemeko ya ardhi Kongo na Rwanda

4 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1rX

KIGALI:

Si chini ya watu 40 wameuawa katika mitetemeko miwili ya ardhi iliyotokea nchini Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo siku ya Jumapili.Zaidi ya watu 500 wamejeruhiwa katika mitetemeko iliyotokea kwenye ukingo wa magharibi wa Bonde la Ufa Mkuu.Kiini cha tetemeko la kwanza kilikuwa nchini Kongo.Tetemeko hilo lilikuwa na kipimo cha 6.0 kwenye Mizani ya Richter.Maafisa wa tume za walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo wamesema,majengo mengi yamebomoka katika mji wa Bukavu.Tetemeko jingine lilitokea upande wa pili wa mpaka nchini Rwanda.