1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Andrea Schmidt24 Septemba 2009

Obama asema lazima wote washirikiane kukabili changamoto la dunia.

https://p.dw.com/p/Jnlu
Rais Barack Obama.Picha: AP

NEW YORK:
Rais Barack Obama wa Marekani ametoa mwito  juu ya kusimama  pamoja katika kuzikabili changamoto kubwa za dunia.

Akilihutubia Baraza  Kuu ya Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza tokea aingie madarakani,  Obama  amesema  jumuiya  ya kimataifa inapaswa  kushirikiana  katika kuzikabili changamoto hizo.  

 Amesema Marekani peke yake haitaweza kutatua matatizo yote ya dunia. Amezitaka nchi ambazo  zimekuwa  zinaikosoa Marekani kwa kupitisha  maamuzi pake yake , sasa kutosimama kando  wakati Marekani ikitatua matatizo. Amesema wakati  sasa umefika kwa wote kutimiza wajibu wao.

Rais Obama amezitaja changamoto zinazoikabili  dunia kuwa  pamoja  na hatari ya silaha za nyuklia,  vita, tishio linalotokana na mabadiliko ya hali ya  hewa na mgogoro wa uchumi.