1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Afghanistan

Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP13 Februari 2009

Richard Holbrooke awasili nchini Afghanistan

https://p.dw.com/p/GtKp
Mjumbe maalum wa Marekani nchini Afghanistan na Pakistan Richard Holbrooke.Picha: picture-alliance/ dpa

Mjumbe maalum wa marekani Richard Holbrooke anatazamiwa kukutana na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama nchini Afghanistan, katika mwanzo wa ziara yake ya siku tatu ya kuthamini hali ilivyo nchini humo. Mjumbe huyo maalum wa Marekani nchini Afghanistan na Pakistan anakabiliwa na kibarua kigumu hasa ikizingatiwa ni majuzi tu wanamgambo wa Taliban walifanikiwa kujipenyeza katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul na kuua watu 26.


Holbrooke amewasili katika mji wa Kabul baada ya ziara yake ya siku nne nchini Pakistan. Hadi kufikia sasa amebakia kimya kuhusu ziara yake katika kanda hiyo ya mgogoro, na jukumu lake jipya kama mshauri wa rais Barrack Obama katika kanda hiyo.


Katika siku yake ya kwanza Afghanistan, Holbrooke anatazamiwa kukutana na waziri wa ulinzi na mkuu wa kitaifa wa shirika la ujasusi nchini humo kabla ya kukutana na rais Hamid Karzai siku ya jumamosi. Mkuu huyo wa shirika la ujasusi nchini Afghanistan bw Amerullah Saleh hata hivyo amekiri hali ya usalama ni tete nchini humo, kwani wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakifanya mashambulizi wapendavyo.

Jukumu kuu la Holbrooke ni kutafuta njisi ya kukabiliana wanagambo hao wa Taliban ambao maficho yao ni kusini mwa nchi hiyo. Huku Marekani ikifikiria kuongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Afghanistan, bado inaona swala hilo si suluhu la mgogoro huo na changamoto kubwa ni kuhakikisha kuwepo kwa utawala wenye kufaa kwa taifa hilo ambalo limekabiliwa na mapigano kwa karibu miaka 30. Amerullah Saleh mkuu wa shirika la ujasusi nchini Aghanistan.


Bw Holbrooke amesema juhudi zake pia zitaelekezwa katika kujaribu kupunguza uhasama kati ya Pakistan na India amatifa ambayo yamekuwa yakichochea vita nchini Afghanistan.Holbrooke ambaye anafahamika kwa kufanikisha kumalizwa kwa mapigano nchini Bosnia amekiri kuwa anakabiliwa na kibarua kigumu nchini humo kuliko hata Iraq.



Hali ya Usalama uliimarishwa kabla ya ziara yake nchini Afghanistan baada ya mashambulizi matatu ya bomu katika majengo ya serikali mjini Kabul na watu waliokuwa na silaha ,tukio ililosababisha vifo vya watu 26.


Mashambulizi nchini Afghanistan yameongezeka tangu majeshi ya marekani kuingia nchini humo kukabiliana na wanamgambo wa Talibam mwaka 2001. Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa matiafa karibu watu elfu 5 wamefariki wakiwemo raia elfu mbili katika mapigano hayo mwaka jana.