1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ajiuzulu

17 Aprili 2024

Abdoulaye Bathily amejiuzulu katika wadhifa wake, akisema shirika hilo la kimataifa haliwezi kufanikiwa kuunga mkono mabadiliko ya kisiasa ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4esX1
Abdoulaye Bathily mjumbe maalum wa Umoja wa Matifa kwa Libya ajiuzulu
Abdoulaye Bathily mjumbe maalum wa Umoja wa Matifa kwa Libya ajiuzuluPicha: Yousef Murad/AP Photo/picture alliance

Bathily ambaye ni waziri wa zamani wa Senegal ameyasema hayo katika kikao na waandishi habari baada ya mkutano wa Baraza la Usalama ambapo alielezea hali ilivyo mbaya katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, iliyokumbwa na mzozo na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya muongo mmoja.

Bathily amesema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya - UNSMIL ulifanya juhudi nyingi chini ya uongozi wake katika kipindi cha miezi 18 iliyopita lakini hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na ukosefu wa dhamira ya kisiasa na nia njema kutoka kwa viongozi wa Libya, huku akisema kuwa hali hiyo ni ya kuhuzunisha kwa sababu idadi kubwa ya watu wa Libya wanatamani kuona mzozo huo ukimalizika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekubali uamuzi wa kujiuzulu kwa Bathily na kumshukuru kwa juhudi zake za kurejesha amani na utulivu nchini Libya.