1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutanao wa Umoja w Mataifa wa Kupambana na Rushwa Duniani

Miraji Othman13 Novemba 2009

Vipi ulaji rushwa utapigwa vita duniani?

https://p.dw.com/p/KWTe
Mwenyekiti wa Shirika la kupambana na ulaji rushwa duniani, Transparency International, Bibi Labelle HuguettePicha: AP

Kutoka Novemba 9 hadi 13 mwaka huu, kutafanyika katika mji mkuu wa Qatar, Doha, mkutano wa nchi zilizotia saini mkataba wa kupambana na ulaji rushwa, UNCAC. Suala la kimsingi la mashauriano ya mkutano huo ni kutaka kuanzishwa duniani kote utaratibu wa kuchunguzana katika jambo hilo.

Serekali za nchi 141 zimetia saini Mkataba wa kupambana na ulaji rushwa, na kati ya hizo zimo nchi 18 ambazo zimo katika orodha ya nchi korofi kabisa katika kwenda kinyume na mapatano hayo: Afghanistan, Haiti, Kirgistan, na Zimbabwe ni chache kati ya hizo. Muhimu ni kutekelezwa mkataba huo na kuchunguza hatua zinazofaa kuchukuliwa:

Mkuu wa Shirika la kupambana na ulaji rushwa duniani, Transparency International, Hugguette Labelle, anasema zile nchi zilizotia saini mkataba huo ziko pamoja. Sasa suala linahusu utaratibu wa kudhibiti na kuchunguza, ili kwamba nchi hizo ziweze kuyatekeleza makubalano hayo. Anasema kwa hivi sasa kuna idadi kubwa ya nchi ambazo hazifanyi hivyo.

Hiyo ndio maana kunafanyika kila mwaka mkutano wa kuuchunguza mkataba huo wa kupambana na ulaji rushwa duniani. Kwa mujibu wa makisio ya Benki ya Dunia ni kwamba nchi zinazoendelea kila mwaka zinapata hasara ya Euro bilioni 25 kutokana na ulaji rushwa au hongo. Mkataba huo wa Umoja wa Mataifa unataoa uwezekano wa kuchukuliwa hatua za kisheria kupambana na uovu huo wa kujitajirisha bila mipaka: akaunti za benki za watu wenye kuendesha mambo hayo zinaweza zikazuiliwa, zikatwaliwa, na fedha zinazohusika katika rushwa hiyo kurejeshewa waliokuw awamilikaji wa fedha hizo. Kutokana na makisio ya benki ya dunia ni kwamba mnamo miaka 15 iliopita karibu Euro bilioni tatu na nusu, ambazo zilipatikana kwa njia isiokuwa ya kisheria, ziligunduliwa na askari kanzu; hiyo ni chembe tu ya mafedha mengi yanayopitiishwa mikoni kwa njia za rushwa. Na ni taabu kwa nchi zunazoendelea kupambana na hali hiyo.

"Jukumu letu ni : Mkataba huo utafikia vipi ili kuzisaidia nchi kuchukuwa hatua sawa ili kuwalinda wananchi wao. Kila mwaka mabilioni ya fedha zizokuwa halali ziko njiani duniani. Hali hiyo inapelekea matumizi ya mabavu, licha ya biashara zizokuwa halali za madawa ya kulevya, usafirishaji usiokuwa halali wa binadamu na vitu kama hivyo. Hiyo ina maana nchi maskini zinabakia kuwa maskini, na watu walio maskini wanalipia gharama kubwa.

Kwa hivyo, ansema Huguette Labelle wa Shirika la Amnesty International, kunahitaji kuweko njia za kisheria ili mapambano dhidi ya ulaji rushwa yafanikiwe. Bila ya kuweko njia za kudhibiti, watu watashindwa kupambana na vita hivyo. Na dhidi ya kudhibiti ulaji rushwa, inaonekana huko Doha, ni baadhi ya nchi ambazo zimeambukizwa sana na ulaji rushwa. Nchi hizo zinataka zenyewe ziwe na dhamana ya kufanya uchunguzi na kuidhibiti hali hiyo na zinazuwia jambo hilo kufanywa na madola mengine au matokeo ya uchunguzi kutangazwa hadharani. Ikiwa hivyo, kwa mujibu wa mkuu huyo wa Transparency International, basi mkataba huo wa Umoja wa Mataifa hautakuwa na thamani hata ya karatasi ulioandikiwa.

Mwandishi:Ulrich Leidholdt/ Miraji Othman/ZR

Mhariri: Mohammed Abdulrahman