1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa Republican wamalizika

Bergmann, Christina 05.09.2008/080904-110465 Septemba 2008

Siku ya Alhamis chama cha Republican nchini Marekani kilimteua seneta John McCain kuwa mgombea wa chama hicho katika kiti cha urais.

https://p.dw.com/p/FCBj
Mgombea wa urais wa chama cha Republican John McCain akiungana na mgombea mwenza Sarah Palin mwishoni mwa hotuba yake ya kukubali kuteuliwa rasmi kuwa mgombea katika mkutano mkuu wa chama cha Republican.Picha: AP



Siku ya Alhamis chama cha Republican nchini Marekani kilimteua rasmi seneta John McCain mwenye umri wa miaka 72 kuwa mgombea wa chama hicho katika kiti cha urais. katika hotuba yake mjini St. Paul jimboni Minnesota McCain aliigawa hotuba yake katika kadha. Hali ya kiuchumi, ambayo ni mada kuu kwa wapigakura, aliikwepa kwa muda. Pia hakujitofautisha sana , kama inavyotarajiwa na rais Bush. Pamoja na hayo hali haikuwa mbaya sana. Maoni ya wapiga kura miezi miwili kabla ya uchaguzi kati ya Barack Obama na John McCain yanaendelea kuwa karibu sawa.


Mac amerejea - Mwaka mmoja nyuma ilionekana kuwa mapambano ya McCain kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi yamefikia mwisho.

Fedha pamoja na mivutano katika timu yake ya kampeni viliingilia kati kampeni yake, na seneta huyo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa karibu kuachia ngazi.

Aliendelea kupambana pamoja na matatizo hayo, na kufanikiwa kupata uteuzi wa chama chake kuwa mgombea, licha ya kuwa kundi la wahafidhina katika chama hicho linaendelea kuwa na shaka.

Hivi sasa lakini Wakristo wenye msimamo mkali nchini humo wanashangilia pia. Sababu ni kwamba , mgombea mwenza wa McCain ni Sarah Palin. Gavana huyo mwenye umri wa miaka 44 kutoka Alaska amejionyesha kuwa ni nyota katika mkutano huo mkuu wa chama cha Republican mjini St.Paul.

Kwanza ni mahesabu aliyopiga McCain. Alitafuta mtu ambae hana doa, ambae anaweza kufanya nae kazi pamoja kuishughulisha serikali mjini Washington.

Ni kura ngapi anaweza kuzipata kutoka kwa Sarah palin, ni lazima kwanza aonyeshe. Wapiga kura wanawake ambao walikuwa upande wa Hillary Clinton sio lazima kuwa watabadilika na kuwa upande wa chama cha Republican, wapiga kura hawa walitaka mgombea mwanamke.

Msimamo mkali wa Palin wa kupinga utoaji mimba, anayefuata kwa dhati dini na upinzani wake dhidi ya elimu kuhusu ngono ni baadhi ya maeneo , ambayo anapingana na seneta wa chama cha Demokratic Hillary Clinton. Kwa mtazamo Sarah Palin halingani kabisa na seneta Clinton ambaye pia alikuwa mke wa rais wa Marekani.

Gavana huyo wa jimbo la Alaska alichukua jukumu la mshambuliaji katika mkutano huo mkuu wa chama cha Republican lakini hajakwenda kombo.

Katika jukumu hilo la mbwa mkali, lakini mwenye kutia rangi ya mdomo kama alivyojionesha , ilijionesha pia kuwa ni mwanasiasa mkali. Aliwashangaza wajumbe wengi wa mkutano huo kwa mashambulizi yake makali dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic Barack Obama. Kama John McCain alivyoahidi kwamba kampeni hazitakuwa chafu, mashambulizi binafsi dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic yanamuangusha.

Pamoja na hayo lakini hotuba hiyo haikutokana na kalamu ya Palin , bali iliandikwa na mshauri wa rais George W. Bush.

Hotuba ya John McCain binafsi ilionesha lugha ya kuvumiliana zaidi . Amesema anamheshimu Obama na kumtambua na amedokeza kuwa yeye pamoja na Obama wangekuwa pamoja zaidi badala ya kutengana.

Mtazamo huu ulionekana vizuri usoni pa McCain. Lakini wajumbe wa mkutano huo walisita kupiga makofi, wanaona mbinu ya mapambano zaidi katika kampeni ya uchaguzi kuwa ni bora. Hii inasikitisha. Wajumbe pia walijizuwia kupiga makofi, wakati McCain alipokuwa akizungumza, kwamba siasa za serikali ya Marekani mjini Washington ,zilizo kinyume na matakwa ya wananchi , lazima chama hicho izibadilishe.

Lakini hapo kabla amejiwekea matatizo, alipaswa kujiweka mbali na siasa za kizamani za George W. Bush. Rais huyo amekuwa ni rais ambaye hapendwi na watu wengi kuliko rais mwingine yeyote aliyewahi kuitawala nchi hiyo. hata hivyo ni chama cha Republican ambacho kimekuwa madarakani kwa muda wa miaka minane sasa na kudhibiti baraza la Congress kwa muda wa miaka 14 iliyopita.

Wakati kiongozi wa chama cha Republican anaulaumu utawala huo, ni kama kujitukana wenyewe.



►◄