1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Ebola waanza Geneva

Admin.WagnerD4 Septemba 2014

Shirila la Afya Ulimwenguni WHO leo hii limeanza mkutano wake wa ndani wa siku mbili mjini Geneva, Uswis wenye lengo la kujadili tiba na chanjo zenye uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola

https://p.dw.com/p/1D6Lf
Ebola in Liberia (Behandlung im Krankenhaus)
Jitihada za kukabiliana na Ebola LiberiaPicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi kutoka mataifa ya Afrika Magharibi pamoja na wataalamu wengine kutoka katika fani za ufamasia, sheria na kutoka katika mamlaka za udhibiti.

Mataifa ya Afrika Magharibi yanapambana kudhibiti kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola, huku shirika la madaktari wasio na mipaka wiki hii likionya kwamba dunia inashindwa kukabilina na vita dhidi ya ugonjwa huo. Onyo hilo linatolewa kukiwa vilevile na habari njema za yule mgonjwa wa aliyetibiwa na dawa aina ya ZMapp akitolewa hospitali baada ya kupata unafuu.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya dola milioni 600 zinahitaji katika kukabiliana na mripuko wa ugonjwa huo katika maeneo ya Afrika Magharibi ambapo hadi sasa idadi yake ya vifo imefikia watu 1,900 na Guinea ikionya kuwa ugonjwa huo vilevile umejipenyeza katika eneo lingine jipya la taifa hilo.

Ongezeko la kiwango cha maambukizi

Serikali nchini Guinea imesema kiwango cha maambukizi kimezidi kuongezeka na kwamba idadi ya vifo ilikuwa inakaribia 400 katika kipindi cha wiki iliyopita. Kwa mara ya kwanza kabisa kadhia hiyo iliweza kubainika katika msitu mkubwa wa kusini/mashariki mwa taifa hilo mwezi Machi.

Kampagne gegen Ebola in Guinea-Bissau
Kampeni ya kukabiliana na Ebola Guinea-BissauPicha: DW/B. Darame

Homa kali ya ugonjwa huo umesambaa kuanzia Liberia, Siera Leone, Guinea Nigeria na Senegal na umesababisha idadi kubwa vifo kuliko awamu zote za mripuko wake tangu ulipotokea kwa mara ya kwanza kabisa 1976 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wakati huo ikijulikana kama Zaire. Mpaka sasa hakuna chanjo wala tiba iliyothibitihwa rasmi.

Dawa ya majaribio kuwasilishwa WHO

Majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo ambayo Canada imesema itauwasilisha kwa WHO kwa ajili ya matumizi ya Afrika bado yapo maktaba katika mchakato mbalimbali ya uendelezaji wake sambamba na namna ya usafirishaji wake.

Kwa hakika jaribio la mwanzo la tiba linatajwa pengine kuanza wiki hii ambapo chanjo kutoka makampuni Glaxo SmithKline na NewLink Genenitc Corp inaweza kutumika.

Kitengo cha Afya na Huduma za Kiutu cha Marekani Jumanne hii kilisema wameingia mktaba ya thamani ya dola milioni 42, kwa lengo la kufanikisha majaribio na ya dawa ilivumbuliwa kapuni ya kibinafsi ya Mapp Biopharceutical Inc.

David Nabalo mratibu mwaandamizi wa Umoja wa Matiafa katika anaeshughulikia ugonjwa huo amesema gharama za fedha zinazohitajika katika kufanikisha hatua mbalimbali za kinga na nita zinaweza kufikia dola milioni 600. Kiwango hicho ni kikubwa kuliko kile kilichokadiriwa awali na WHO cha dola milioni 490 wiki iliyopita.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga