1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele kuhusu Afrika

Sekione Kitojo
14 Juni 2017

Wahariri wa magazeti ya hapa Ujerumani(14.06.2017)wamejishughulisha zaidi na mada kuhusu mkutano wa kilele kuhusu bara la Afrika, mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa majimbo ya Ujerumani kuhusu hali ya usalama. 

https://p.dw.com/p/2egWw
Deutschland G20 Afrika Treffen
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Mada nyingine ni  kuhusu jinsi alivyohojiwa mwanasheria  mkuu  wa  Marekani Jeff Sessions  na  kamati  ya baraza  la  Seneti  hapo  jana.

 

Mada  kuhusu  mkutano  wa  kilele  kuhusu  bara  la Afrika  uliomalizika  jana  mjini  Berlin hapa  Ujerumani. Mhariri  wa gazeti  la  Die Rheipfalz anaandika  kwamba , kwanini  misaada  ya maendeleo  haileti  maendeleo? Mhariri  anaendelea  kuandika 

 

"Ni  kwasababu  , kwanza ; Ni wanasiasa pekee  na  wale wenye uwezo  kiuchumi ndio  wanafaidika  zaidi  katika  nchi  hizo zinazopokea  misaada. Kwa wale  mamilioni  ya  Waafrika  ambao wakati  wote  wako katika  hali  ngumu  ya  maisha  hawapati chochote. Kwa  upande  wa  nchi  wafadhili , kitengo  cha  misaada ya  maendeleo , ni  chombo  cha  kujinufaisha. Ndio  sababu  juhudi za  Merkel  zina kiini  cha  kushindwa, kwa  kuwa  hazihusiani  kabisa na  maendeleo. Ukweli  ni  kwamba  wanataka  kuwazuwia  watu wanaotaka  kuhama  kutoka  bara  la  Afrika  kuja  Ulaya.  Unaweza mtu  kusema  hilo, na  Merkel  anapaswa  kusema  hivyo  sio  kujaribu kuleta  matumaini  ambayo  hayapo."

Deutschland G20 Afrika Treffen
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Msingi  wa  hamasa  mpya  kuhusu  bara  la  Afrika  ni  nyingine kabisa, anaandika  mhariri  wa  gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung  kuhusiana  na  mkutano  huo  wa  kilele  kwa  ajili  ya  bara la  Afrika. Mhariri  anaendelea ....

 

"Ni  kuhusu kuzuwia  uhamiaji. Waafrika  hawatakiwi  kuja  kwetu, wanatakiwa  kutafuta kazi  katika  nchi  zao na  wabakie  huko. Ndivyo  wanavyofikiri  watu  wa huku  kaskazini. Utaratibu  sio kuwakataa  kabisa , lakini  umo  katika  makosa  yetu. Ukuaji  wa uchumi  hautazuwia  uhamiaji, badala  yake  unahimiza. Waafrika wengi  wamehamia  nchi  za  nje  katika  wakati  wa  ukuaji mkubwa wa  uchumi  hivi  karibuni  kuliko  wakati  mwingine  wowote. Ghana , Senegal , Nigeria,  si  kitu  cha  bahati  mbaya  kwamba  watu  wengi walioomba  hifadhi  wanatoka  nchi  hizi zilizoneemeka. Masikini wengi  hawana fedha  ama  nguvu  za  kuweza  kufanya  safari  za kuhamia nchi  za  nje.  Inahitaji  zaidi  ya  ukuaji  wa  uchumi , kwa watu  kubakia katika  nchi  zao. Wakati  kundi  la  G20 linalenga kuwekeza  katika  sekta  binafsi  kama  nguvu  ya  kuleta  maendeleo katika  bara  la  Afrika, haina  maana  ya  kuondoa kiini  cha matatizo , ambayo ni rushwa."

Deutschland G20 Afrika Treffen
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Kuhusu mada  ya  mkutano  wa  mawaziri  wa  mambo  ya  ndani  wa serikali  za  majimbo  nchini  Ujerumani  kuzungumzia  kuhusu usalama  wa  ndani  kabla  ya  uchaguzi  mkuu  mwezi  Septemba , mhariri  wa  gazeti  la  Stuttgarter Zeitung  anaandika:

 

"Sheria  zilizopo  za  usalama  haziwezi  tena  kuufanya  ulimwengu kuwa  salama. Tunapata  uzoefu  huo  na  mawaziri  wa  mambo  ya ndani  kutoka  serikali  kuu na za  majimbo watakuwa  waangalifu sana  kuweza kulichokoza suala  hilo, kwa  kuwa  wakiamua  kuleta sheria  mpya  huenda wakawaweka  wananchi  katika  hali  ngumu. Ni  somo  pia  kutokana  na  tukio lililofanywa  na  mhamiaji  Amri , ambaye  kama sio  kushindwa  kushindwa  kwa  maafisa  wa usalama  kumdhibiti mambo  yaliyotokea  yasingetokea."

 

Gazeti  la  mjini  Mainz  , Allgemeine Zeitung , linaandika  kuhusu mada  hiyo  kwa  kusema..

"Baadhi  ya  nyakati  kunaonekana  wazi  kabisa  hali  ya  udhaifu katika  serikali  ya  shirikisho . Kutokana na  mbinu  zinazotofautiana kwa  maafisa  wa ulinzi  wa  amani   katika  jeshi  la  polisi wamewafanya  wahalifu  kuwa  na  nguvu  zaidi. Hali  hii  imejengeka kwa  miaka  mingi , iwapo  itabadilika, haijulikani. Kila  jimbo  linahitaji sheria  zake  za  jeshi  la  polisi  kuweza  kujilinda, ambazo  zinaweza pia  kutumika  nchi  nzima, utaratibu  wa  adhabu  unaweza kuainishwa na  kuwa  na  nguvu  zaidi."

 

Kuhusu  kuhojiwa  kwa  mwanasheria  mkuu  wa  Marekani  katika kamati  ya  baraza  la  seneti  jana , mhariri  wa  gazeti  la Landeszeitung  la  mjini  Lüneburg  anaandika ......

Jeff Sessions USA Anhörung
Mwanasheria mkuu wa serikali ya Marekani Jeff SessionsPicha: Getty Images/S.Loeb

"Kabla  hata  mwanasheria  mkuu  wa  serikali  ya  Marekani  Jeff Sessisions kusema  kitu  ilikuwa  tayari  ni  wazi , kwamba atabadilisha  mwelekeo wa  athari zinazotokana  na Trump. Mwelekeo  ni  kuhusu mchanganyiko  wa  madaraka  yake  kama rais  na  biashara  zake  za  mahoteli. Kama  kutakuwa  na mashitaka , huenda  Trump  akalazimishwa  kuweka  wazi marejesho ya  matumizi  yake  pamoja  na  kodi.  Hii  inapelekea  kuwapo  na fursa  ya  kumshitaki.  Na  hapa  panahitajika  theluthi  mbili  ya wabunge  wa  baraza  la  seneti. Lakini   wabunge  wa  chama  cha republikan  ambao  hawamtetei  Trump  ni  wengi  pia. Hii  ni kutokana  na  sababu  moja  muhimu. haijawahi  kutokea  wananchi wengi  wa  Marekani  katika  muda  mfupi  tangu  rais  kuingia madarakani  kuwa hawana imani  na  kazi  yake."

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Yusuf Saumu