1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi wamalizika Vienna

Josephat Nyiro Charo23 Julai 2010

Changamoto zingalipo katika kutafuta tiba na chanjo dhidi ya janga la ukimwi duniani

https://p.dw.com/p/OTQw
Mjumbe kwenye mkutano wa ukimwi wa Vienna akitazama mabango kuhusu ukimwiPicha: picture alliance / dpa

Nchini Austria, mkutano wa 18 wa kimataifa uliyoyajadili masuala ya Ukimwi umekamilika.Kikao hicho kilichoanza Jumapili iliyopita kiliwaleta pamoja wataalam na wanaharakati wa masuala ya Ukimwi.Katika sherehe rasmi za kukifunga kikao hicho, Rais Obama ameahidi kuziimarisha juhudi za nchi yake katika vita dhidi ya Ukimwi.

Katika hotuba yake iliyorushwa kwa video, Rais Obama alisema kuwa juhudi zao za vita hivyo zitaimarishwa kwa manufaa ya wote. Moja ya masuala muhimu yaliyojadiliwa Vienna ni dawa za kupambana na makali ya Ukimwi,utafiti wa chanjo,pesa za ufadhili na malham mpya iliyovumbuliwa.

Jee mtu anayeishi na virusi vya HIV ana mtazamo gani? Thelma Mwadzaya amezungumza na Bi Huruka Mohammed, mkaazi wa Dar es salaam,Tanzania, ambaye amekuwa akiishi na virusi vya HIV kwa miaka 21.