1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani mjini Nürnberg

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsH

Nürnberg:

Mawaziri wa mambo ya ndani wa serikali kuu na wa majimbo ya Ujerumani wanaanza kukutana hii leo kwa mazungumzo ya siku mbili mjini Nürnberg.Mada kuu mazungumzoni ni kuhusu mvutano uliosababishwa na maridhiano yaliyofikiwa na serikali kuu kuhusu haki ya kuishi humu nchini wageni waliokua wanavumiliwa tangu muda mrefu uliopita.Hasa majimbo ya Niedersachsen na Bayern ndiyo yanayoyatia ila maridhiano hayo.Viongozi wa majimbo hayo mawili yanayoongozwa na vyama ndugu vya CDU/CSU wanahofia zaidi maridhiano hayo yasije yakageuka mzigo kwa mfumo wa huduma za jamii.

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble anawahimiza viongozi wakubali kuunga mkono maridhiano hayo.Bwana Schäuble anasema:

"anaamini kwamba watu wanaoishi humu nchini ,naiwe wana asili ya kigeni au la,hawawezi kutegemea viongozi wa kisiasa watajadiliana tuu,bali watataka kuwaona wakiyapatia ufumbuzi hata yale masuala ambayo ni tete.”

Maridhiano hayo ya serikali kuu yanazungumzia juu ya kupatia haki ya kuishi wageni ambao hadi sasa wamekua wakivumiliwa,kwa sharti lakini wanafanya kazi..