1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mwaka wa bunge la China

Abdulrahman, Mohamed5 Machi 2008

Waziri mkuu Wen Jiabao afafanua juu ya hali ya kiuchumi ya taifa hilo kubwa barani Asia.

https://p.dw.com/p/DIJG
Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao.Picha: AP

Akilihutubia bunge hilo Waziri mkuu Wen Jiabao amesisitiza kwamba zingatio kubwa hivi sasa ni kupambana na ughali wa maisha. Paia amesema matatizo ya kiuchumi nchini Marekani na kwengineko yanaathari zake kwa China yenye jumla ya wakaazi bilioni 1.3 na kwamba serikali yake itachukua hatua kupunguza kasi ya ukuaji uchumi hadi 8 asili mia mwaka huu, kutoka asili mia 11 .4 mwaka jana na kuzuwia kupanda bei za bidhaa zaidi ya 4.8 asili mia

Lakini waziri mkuu huyo alikiri kwamba kupambana na ughali wa maisha kutakua kugumu baada ya mwaka jana wa 2007 kushuhudiwa kupanda mno kwa chakula na mahitaji muhimu na kuzusha hali ya wananchi kutoridhika na serikali.

Bw Wen aliwaambia wajumbe wapatao 3,000 wa bunge hilo la taifa kwamba kupanda kwa bei na kuongezeka kwa ughali wa maisha ndiyo tatizo kubwa linalowakabili wananchi wa nchi hiyo kwa wakati huu na kuwa shinikizo dhidi ya mfumko wa bei litabakia kuwa kubwa mwaka huu.

Hali hiyo imekua ni ya wasi wasi kwa watawala wa kikoministi nchini China kwa sababu mara nyingi huweza kuzusha ukosefu wa utulivu katika jamii.

Mbali na ughali wa maisha waziri mkuu Wen alisema pia kipa umbele kwa serikali katika sekta ya uchumi ni kuzuwia ukuaji uchumi kuwa mkubwa kupita kiasi. China imeweka lengo la ukuaji uchumi wa kiwango cha 8 asili mia lakini kimekua kikiongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka mitano mfululizo.

Akizungumzia juu ya changa moto kutoka nchi za nje, ukiwemo msuko suko wa kiuchumi nchini Marekani na kitisho cha kuchukuliwa hatua za kujilinda kibiashara,Bw Wen alitaja juu ya tatizo la mkopo wa majumba nchini Marekani na wengi kushindwa kulipa kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, pamoja na kuzidi kuanguka kwa dhamani ya sarafu ya dola, kuwa miongoni mwa changa moto kubwa kwa uchumi wa China.

Matokeo yake ni kuongezeka pia kwa mabishano na mfarakano wa kibiashara.Mwezi Julai 2005, China ilijiondoa katika mfumo wa fedha wa sarafu yake ya Yuan katika soko la ubadilishanaji sarafu kulingana na dola ya Marekani, na kuicha itegeme kiwango cha ubadilishaji kilivyo katika masoko.

Wakati yote hayo ni sehemu ya mageuzi nchini China, Bw Jin mhariri wa gazeti jarida la OPEN yaani Uwazi linalotoka mjini Hong Kong, anasema tatizo ni ukosefu wa uwazi, akifafanua kuwa "Nchini China kama ilivyokua awali, kuna mjadala juu ya mageuzi ya kisiasa na kuhusu tafauti ya msimamo kati ya jumuiya za kiraia na serikali. Maoni ni yenye kutafautiana sana inazidi kuvidhibiti vyombo ya habari ya dola."

China inatarajia nakisi katika matumizi yake ya serikali kupungua hadi Yuan bilioni 180 sawa na dola bilioni 25.4 mwaka huu, ikiwa ni upungufu wa asili mia 27 kutoka mwaka uliopita 2007.


Wataalamu wa masuala ya uchumi hata hivyo wanasema wana shaka shaka kama kweli maneno ya Bw Wen yataweaza kwa njia yoyote kwenda sambamba na kuidhibitiwa kwa sera za serikali yake.

Kwa mfano wanasema saula la ughali wa maisha linatokana na usambazaji bidhaa usiokua wa kutosha, kwa hivyo lengo linapaswa kuwa ni kuimarisha usambazaji huo .