1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Republican

3 Septemba 2008

Mkutano wa chama tawala cha republic nchini Marekani utamuidhinisha rasmi leo Seneta McCain.

https://p.dw.com/p/FAXy
John McCain na mwenzake Sarah Palin.Picha: AP

Mkutano mkuu wa chama-tawala cha Republican ukitazamiwa leo kumtawaza Seneta John McCain kuwa mtetezi wake wa uchaguzi ujao wa urais.Rais George Bush, alimueleza mtetezi huyo kuwa ni mtu aliejifunza darasa la shambulio la Septemba 11, 2001 na kwamba ndie anaefaa kuwa rais mpya wa Marekani.

►◄

Rais George Bush ambae umaarufu wake umepungua mno na kupelekea asiweze kumpigia debe sana Seneta John McCain mkutanoni huko Minnesota,alivunja ziara yake ya Minnesota kutokana na kimbunga Gustav kilichovuma katika pwani ya Ghuba la Marekani.

Bush alimueleza John McCain kuwa ni mtu anejiamulia mambo kwa jinsi aonavyo yeye na mwenye uwezo wa kuiongoza Marekani katika kipindi cha vita.Akakumbusha historia ya kijeshi ya John McCain wakati wa vita vya Vietnam akiwa rubani hadi kupelekea kukamatwa kwake na kuteswa akiwa kifungoni kwa miaka 5 gerezani Hanoi.

Rais Bush alisema bila ya kuwapo mkutanoni kwamba, walimwengu wanaishi kipindi kigumu:

"Tunamhitaji rais anaeelewa darasa la shambulio la Septemba 11,2001.Kwamba kuilinda Marekani,lazima tuwe macho na kuzuwia hujuma kabla kutokea-mtu tunaemhitaji kwa hayo ni John McCain."

Alisema rais Bush.

Mjumbe wa Arizona mkutanoni Augustus Shaw alisema hakuvunjika moyo kwa Geroge Bush kutohudhuria mkutano huu wa chama cha Republican huko Minnesota. Akaongeza na ninamnukulu,

"Yeye ni rais wa Marekani na sasa tumekabili msukosuko wa kitaifa -kimbunga cha huko Mississippi.Kwa kweli, ningeingiwa na wasi wasi laiti angelikuwapo hapa mkutanoni wakati huu..."

Shaw,mwanasheria mkuu wa Arizona aliungama kwamba kutohudhuria kwa George Bush mkutano huu unaomurikwa na vyombo vingi vya TV,huenda kukamsaidia seneta McCain.

Hotuba ya Bush ameitoa siku ya pili ya mkutano huu wa chama-tawala cha Republican ambao ulipunguzwa kasi yake mno jana kutokana na msukosuko wa kimbunga cha Gustav.

Wajumbe mkutanoni wanatarajiwa kumpitisha rasmi leo usiku nae MacCain atazamiwa kutoa hutuba yake ya kupokea jukumu hilo hapo kesho.

Warepublican wamekuwa wakimbomoa mtetezi wa chama cha democratic party Seneta barack Obama aliechaguliwa katika Baraza la senate 2004 na kwamba eti hana maarifa ya kutosha kuweza kuiongoza Marekani.

Usiku wa hotuba ya Bush ulichangiwa na hotuba za seneta anaejitegemea mwenyewe Joe Liebermann,wakati mmoja alikuwa mwanachama wa democratic party na mgombea-mwenza wa kiti cha urais.

Liebermann,rafiki wa chanda na pete wa John McCain,zamani alimueleza Obama:

"Seneta Barack Obama ni kijana mwerevu na mzungumzaji fasaha.Natuami aweza akaifanyia makubwa nchi yetu miaka ijayo.

Ufasaha pekee haujazi pengo la rekodi ya utendaji na hasa si wakati huu mgumu."

Wajumbe mkutanoni walizungumzia maswali ambayo Seneta MCCain akivutana sana na rais Bush aliepoteza heba yake-sera za kodi,uhamiaji na kuongezwa majeshi Irak ambako Mccain alikuongamkono na kuwa sera iliofanikiwa.

Tangu Bush kumuidhinisha McCain hapo machi mwaka huu,Seneta McCain alijitokeza hadharani mara moja tu na rais Bush na ilikuwa katika hafla ya faragha ya kukusanya michango.

Wakati geroge Bush hakuweza kuhudhuria mkutano huu huko Minnesota, baba yake na rais wa zamani George HW Bush pamoja na mkewe Barbara walimehudhuria.