1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Serbia na Kosovo umemalizika bila maafikiano

Sudi Mnette
19 Agosti 2022

Viongozi wa Serbia na Kosovo, Jana Alhamisi wameshindwa kufikia makubaliano ya mgogoro wa muda mrefu wa kimipaka na suala la utambuzi, masuala ambayo yamezusha mvutano katika eneo la Balkan.

https://p.dw.com/p/4Fkyd
Spannungen zwischen Kosovo und Serbien
Picha: Visar Kryeziu/AP/picture alliance

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti walifanya mazungumzo mjini Brussels wakati wa mkutano ambao ofisi ya mahusiano ya kigeni ya Umoja wa Ulaya ilisema ulifanyika katika wito wa dharura.

Baada ya mkutano huo mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell baadae alijitokea na kutangaza kuwa hakukuwa na maafikiano yoyote. Zaidi alisema "Lakini wamekubaliana kuondelea na majadiliano ya mara kwa mara katika kipindi kijacho, ili kurejesha hali ya utulivu haraka, haraka. Na ntalipa kipaumbele hili katikia ajenda yangu kwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya."

Ukimya wa viongozi mahasimu baada ya mkutano.

Konflikt zwischen Serbien und dem Kosovo Josep Borrell
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep BorrellPicha: Virginia Mayo/dpa/picture alliance

Hakukuwa na kauli yoyote kutoka kwa Vucic wala Kurt. Lakini vyombo vya habari vya Serbia vilitangaza kuwa Vucic  atalihutubia taifa baadae leo.

Kosovo ni jimbo la zamani la Serbia ambalo limekataa tamko la utambuzi wa uhuru wa taifa hilo mwaka 2008. Mwaka 1999, uingiliaji wa vikosi vya Jumuiya ya Kujihami ya NATO, ilishiriki uvamizi ambao ulivifikisha vita kati ya jeshi la Serbia na wanaotka kujitenga huko Kosovo, na kadhalika kufanikisha kudhibiti ukandamizaji uliogharimu maisha ya wengi wa Balgrade didi ya jamii ya waliowengi ya Waalbania wa Kosovo.

Jitihada ya Umoja wa Ulaya katika mzozo wa Serbia na Kosovo.

Kwa muda mrefu Umoja wa Ulaya umekuwa ukisimamia mazungumo ya kurejesha hali ya utulivu kwa pande hasimu, kwa kusema hatua hiyo ni sehemu ya sharti kuu ambalo lingeweza kuzifanya Kosovo na Serbia kufanikiwa kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya wenye mataifa wanachama 27.

Lakini haya mazungumzo ya Alhamis, pamoja na nia hiyo Borrell alisema yalikuwa na nia ya kutuliza hali ilivyo katika maeno hayo.

Mvutano kati ya Serbia na Kosovo ulishika kasi  upya mwishoni mwa mwezi uliopita pale ambapo serikali ya Waziri Mkuu Kurti ilipotangaza hati za utambulisho kwa Serbia na leseni za mamba za magari hazitatuma katika eneo la Kosovo.

Soma zaidi:Scholz azitaka Kosovo na Serbia kutafuta amani

Kwa upande wake Serbia imekuwa ikitekeleza hatua sawa kwa raia wa Kosovo ambao wameingia katika mipaka yaje ndani katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Ikisema ikiwa inatambuwa usajili wa magari ya Kosovo na nyaraka za utambuzi za watu wake, ni sawa na kuitambua Kosovo kama nchi huru.

Chanzo: AP