1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa usalama wamalizika

10 Februari 2008

Wito watolewa kwa jumuiya ya kimataifa kukabiliana na kitisho cha Nuklia

https://p.dw.com/p/D58o

MUNICH

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ameitaka jumuiya ya kimataifa kuweka mbele suala la kukomesha harakati za kuenea kwa Nuklia pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa Nishati.Waziri Steinmeier ameyasema hayo hapo jana katika mkutano wa 44 wa kimataifa juu ya usalama mjini Munic ambapo pia amesisitiza kuhusu kuendelea kujitolea kwa Ujerumani katika juhudi za kuweka usalama nchini Afghanstan.Akiyajibu matamshi ya waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates kwamba Ujerumani ikihamishe kikosi chake cha wanajeshi 3200 kutoka kaskazini mwa Afghanstan na kukipeleka katika eneo hatari la kusini,waziri Steinmeir amesema Ujerumani inatimiza zaidi ya majukumu yake.

Hata hivyo taarifa zinasema serikali ya kansela Angela Merkel inatafakari juu ya kuongeza wanajeshi nchini Afghanstan inagwa waziri wa Ulinzi Franz Joseph Jung akihutubia mkutano wa Munich amekataa kugusia juu ya suala hilo.Idadi kubwa ya wananchi wa Ujerumani wanapinga hatua ya kutuma majeshi katika eneo la kusini mwa Afghanstan.Ujerumani ni ya tatu yenye idadi kubwa ya wanajeshi katika Afghanstan lakini inapinga hatua ya kutuma wanajeshi wake Kusini.