1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkwamo wa kisiasa Kenya kutatuliwa?

Thelma mwadzaya9 Agosti 2023

Viongozi wa serikali ya Kenya Kwanza na upinzani wa Azimio la Umoja leo wamerejea kwenye meza ya mazungumzo ya upatanishi, baada ya kupishana juu ya kile walichokiita maslahi chanya ya wakenya.

https://p.dw.com/p/4Uxdw
Kenia Präsident William Ruto
Picha: TONY KARUMBA/AFP

Hii ni mara ya pili vikao hivyo vya pamoja kufanyika baada ya kuvunjika Aprili na upinzani kufanya maandamano kwa wiki kadhaa.

Ajenda ya kikao bado inazua mitazamo tofauti. Mazungumzo hayo yanafanyika chini ya upatanishi wa rais mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo.

Baada ya miezi kadhaa iliyogubikwa na vurugu za siasa, hatimaye kikosi cha wanachama kumi wa pande zote mbili za serikali ya Kenya Kwanza na upinzani wa Azimio la Umoja wamekutana kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya jijini Nairobi.

Soma pia:Mazungumzo ya kusaka maridhiano Kenya kuanza Jumatano

Upinzani wa Azimio la Umoja unawakilishwa na kinara wa Wiper Demokratik Kalonzo Musyoka aliyesisitiza kuwa maslahi ya Wakenya ndiyo yanayowasukuma.

Upande wa serikali ya Kenya Kwanza unawakilishwa na kiongozi wa wengi bungeni, Kimani Ichungwah.

Mapema akiwa eneo la Naro Moru la kaunti ya Nyeri akimsindikiza Rais William Rutoalishikilia kuwa wako ngangari.

Hakuna mgawanyo wa madaraka

Kwenye kikao hicho, gavana wa kaunti ya Embu Cecily Mbarire alibainisha kuwa mustakabal wa nchi ndio jambo la msingi na hawana budi ila kuheshimu katiba.

Ajenda ya kikao bado inazua mitazamo tofautinje na ndani ya serikali ila kilicho bayana ni kuwa hakuna kugawana madaraka.

Ifahamike kuwa Rais William Ruto yuko ziarani eneo la Mlima Kenya na ameziafiki kauli hizo.Mazungumzo ya kusaka maridhiano Kenya kuanza Jumatano

Masuala yanayozua utata ni uteuzi wa makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, ushirikiano kuhusu masuala ya taifa, nafasi ya upinzani katika uongozi rasmi na utekelezaji wa sheria ya usawa wa kjinsia.

Polisi Kenya yazuia maandamano ya upinzani

Soma pia:Obasanjo aingia kati kuwapatanisha Ruto, Raila

Upinzani unashikilia kuwa gharama za maisha zilizoongezeka zinahitaji mjadala wa kitaifa na kuona namna gani kata nchi wanaweza kutatua.

Ikumbukwe kuwakesi ya kupinga sheria ya fedha ya 2023 itakayowabinya Wakenya wakati inaiongezea serikali pato kupitia nyongeza ya kodi.

Kwa sasa jaji aliyesitisha utekelezaji wa sheria hiyo Mugure Thande amehamishiwa mahakama ya Malindi kutokea Nairobi.

Jaji David Majanja ambaye ni mmoja ya watatu watakaosikiliza kesi hiyo naye pia ameondolewa kwenye kitengo cha masuala ya kodi katika mahakama ya Milimani.

Mazungumzo yataanza rasmi wiki ijayo.