1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

​​​​​​​Mo Farah kuhamia mbio za marathon

Bruce Amani
21 Agosti 2017

Mo Farah ameshusha pazia la taaluma yake ya kushiriki mashindano ya ndani mwa uwanja nchini Uingereza, baada ya kushinda mbio zake za mwisho kwenye ardhi ya nyumbani.

https://p.dw.com/p/2iZk9
Leichtathletik WM London 2017- Mo Farah
Picha: Reuters/L. Nicholson

Mbio zake za mwisho zitakuwa Zurich Weltklasse Alhamis wiki hii kabla ya kujitosa katika ulimwengu wa mbio za marathon barabarani msimu ujao. "Bila shaka nna furaha kubwa. Imekuwa safari zunri sana. Kuweza kufanikiwa yote niliyoyapata kwa kipindi cha miaka hiyo yote. Wananimichezo wengi huwa na ndoto ya kuwa bingwa wa Olimpiki na kuwa na medali nne za Olimpiki mfukoni mwangu zikiwa na majina ya wanangu ni heshima kubwa. Na sasa nataka tu kufurahia na kuingia barabarani katika mbio za marathon bila ya kuwa na lengo lolote kichwani. Niwe tu mtulivu, na kushiriki kama mtu mpya na bila kutarajia chochote kutoka kwangu, isipokuwa tu nini ambacho Mo anaweza kufanya? Alisema Farah

Farah mwenye umri wa miaka 34 alishinda fedha katika mbio za mita 5,000 na dhahabu katika mita 10,000 kwenye mashindano ya riadha ya dunia yaliyokamilika hivi karibuni jijini London.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman