1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU :Hakuna mikataba ya kuchimba mafuta asema Waziri mkuu Gedi

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhv

Waziri mkuu wa muda wa Somalia Ali Mohamed Gedi anashikilia kuwa serikali yake haina taarifa kuwa kampuni moja ya Uchina imetia saini mkataba wa kuchimba mafuta.

Kwa mujibu wa mahojiano na gazeti la Financial Times la Uingereza stakabadhi zilizotiwa saini na Rais Abdullahi Yusuf Ahmed wa Somalia linawapa maafisa wawili uwezo wa kutia saini makubaliano kwa niaba ya serikali ya Somalia na kampuni ya Uchina kuchimba mafuta.

Wakati huohuo yapata watu 3 wameuawa katika ghasia mpya mjini Mogadishu.Shambulio hilo limetokea katika soko la Bakara ambapo maafa kadhaa yalitokea wiki jana.Kulingana na walioshuhudia tukio hilo watu wasiojulikana waliwarushia polisi walioshika doria maguruneti katika soko hilo.

Visa hivyo vinatokea siku moja baada ya makombora kushambulia eneo la mkutano wa kutafuta amani ya nchi hiyo.Mkutano huo umeahirishwa hadi siku ya Alhamisi.