1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mashambulio yaendelea mji mkuu wa Somalia

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDk

Mji mkuu wa Somalia,Mogadishu unaendelea kushambuliwa kwa makombora na risasi kwa siku ya tatu kwa mfulululizo.Ripoti zinasema,zaidi ya watu 250 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa raia wa kawaida tu.Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na washirika wao wa Kiethiopia,wanaendelea na mashambulio yao dhidi ya waasi wenye itikadi kali za Kiislamu lakini raia wanalalamika kuwa mji wa Mogadishu unashambuliwa kiholela.Wakazi kwa maelfu wanauhama mji huo mkuu kujiepusha na mapigano makali kabisa kupata kushuhudiwa mjini Mogadishu tangu zaidi ya miaka 15.Kwa mujibu wa halmashauri ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi duniani,katika juma lililopita peke yake kama watu 12,000 wameukimbia mji huo mkuu.Kwa hivyo sasa idadi ya wakimbizi kuanzia mwezi wa Februari imefikia 57,000.