1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU. Wanajeshi wapania kuuteka mji wa Kismayo

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCee
Waziri wa mambo ya kigeni wa mamlaka ya Palestina Ziad Abu Amr (k) akiwa na waziri mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier baada ya mazungumzo yao mjini Berlin hivi karibuni.
Waziri wa mambo ya kigeni wa mamlaka ya Palestina Ziad Abu Amr (k) akiwa na waziri mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier baada ya mazungumzo yao mjini Berlin hivi karibuni.Picha: AP

Serikali ya mpito ya Somalia imesema majeshi yake yanapania kuuteka mji wa bandari wa Kismayo kusini mwa Somalia. Wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia wameanza kuyavamia maeneo yanayomilikiwa na wanamgambo wa mahakama za kiislamu kusini mwa Somalia.

Mji wa bandari wa Kismayo unasemekana umebakia kuwa ngome ya mwisho ya wanamgambo hao walio watiifu kwa mahakama hizo za kiislamu. Wanamgambo hao waliukimbia mji mkuu Mogadishu mnamo Alhamisi iliyopita baada ya kutimuliwa na majeshi ya Somalia na Ethiopia.