1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu.Maafisa wa Pontland wapinga kuhusu kufanyika mapigano.

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvR

Vikosi vya mahakama za kiislamu nchini Somali vimesema vimepambana na wanamgambo wanaoungwa mkono na Ethiopia kaskazini mwa nchi hiyo.

Umoja wa Mahakama za kiislamu umesema vikosi vyake vilishambuliwa karibu na mpaka wa jimbo la Puntland, jimbo lenye mafungamano na Ethiopia na mabalo hadi sasa linakataa kushirikiana na mahakama za kiislamu zinazodhibiti sehemu kubwa ya Somalia na mji mkuu Mogadishu.

Maafisa huko Pontland hata hivyo wamekanusha ripoti za mapigano wakisema, mahakama za kiislamu zinatafuta sababu tu za kulishambulia jimbo lao.

Wakati huo huo maafisa wa Ethiopia wamekanusha kwa mara nyengine tena madai kuwa wametuma wanajeshi nchini Somalia.