1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mapigano makali yazuka Mogadishu watatu wauawa

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBN8

Wanamgambo wa kiislam wamepambana na majeshi ya serikali ya mpito nchini Somalia ambapo watu watatu inaarifiwa kuwa wameuawa katika mapambano hayo yaliyotokea huko kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Mapigano hayo yametokea siku tatu baada ya muungano mpya wa makundi ya kiislam kutangaza kuwa wapiganaji wao wameanzisha mashambulizi kuyafurusha majeshi ya Ethiopea yanayoisadia serikali ya mpito.

Kwa mujibu wa mashuhuda, silaha mbalimbali yakiwemo makombora ya kutungulia ndege zilitumika katika mapigano hayo yaliyotokea karibu na chuo kikuu cha Mogadishu pamoja na makaburi ya Barakat.

Majeshi ya Ethiopea yanayoyasaidia yale ya serikali ya mpito pamoja na kikosi cha askari 1500 wa Umoja wa Afrika ambao ni askari kutoka Uganda wameshindwa kuwadhitibiti wanamgambo hao wa kiislam.