1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mkutano wa maridhiano ya kitaifa wamalizika

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUC

Mkutano wa maridhiano ya kitaifa unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya umemalizika mjini Mogadishu baada ya siku 45 bila mafanikio yoyote.Kikao hicho kilisusiwa na wahusika muhimu wakuu ambao ni wawakilishi wa ukoo wa Hawiye pamoja na wapiganaji wa mahakama za kiislamu jambo lililopelekea vikao kuahirishwa na kusogezwa mbele.

Kulingana na mjumbe mmoja aliyehudhuria kikao hicho wafadhili wa kigeni walitoa ahadi zao ila lengo hasa la mkutano halikufikiwa.Mkutano huo uliazimia kuleta maridhiano ya kitaifa kati ya koo zinazozozana vilevile kudumisha amani mjini Mogadishu.

Mashambulio ya makombora yaliendelea wakati mkutano huo ulipoanza Julai 15 ikiwa ni juhudi za wapiganaji wa kiislamu kuwafurusha majeshi ya Ethiopia yanayounga mkono majeshi ya Somalia kudumisha amani nchini humo.Zaidi ya watu alfu 1 wamepoteza maisha yao katika ghasia hizo.

Somali imekuwa bila serikali tangu mwaka 91 baada ya Mohamed Siad Barre kungolewa madarakani.