1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco mwenyeji mkutano wa AU

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2016

Morocco ndiye mwenyejii wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Afrika katika wakati ambapo taifa hilo likijaribu kurejea kuwa mwanachama wa Umoja wa Afrika baada ya kujiondoa miaka 32 iliyopita. 

https://p.dw.com/p/2Slih
Ruanda Paul Kagame und Mohammed VI
Picha: GettyImages/AFP/S. Aglietti

Takribani viongozi 30 wakuu wa Kiafrika wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa kilele, akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Muhammadu Buhari wa Nigeria.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) pia anahudhuria mkutano huo.

Mkutano huo unafanyika pembezoni mwa mkutano wa kimataifa wa kujadili mabadiliko ya tabia nchi unaoandaliwa na Umoja wa Mataifa mjini Marrakesh.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa anatarajiwa kuwahutubia viongozi hao wa Afrika.

"Mkutano huu ni fursa kwa viongozii wa Afrika kuratibu misimamo yao na kuzungumza kwa kauli moja ili kujilinda", alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar.