1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rais wa Urusi apinga mradi wa Marekani

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GD

Mradi wa Marekani,kutaka kuweka mtambo wa kinga dhidi ya makombora katika nchi za Ulaya ya Mashariki,unazidi kuathiri uhusiano wa Urusi na Marekani.Rais wa Urusi Vladimir Putin alisisitiza upinzani wake kuhusu mradi huo,baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice na Waziri wa Ulinzi Robert Gates.Amesema,Washington inahatarisha uhusiano wake na Moscow,kwa sababu ya mpango huo.

Mwanzoni mwa mkutano,Putin alitishia kujitenga na makubaliano muhimu yaliyotiwa saini kati ya Urusi na Marekani katika mwaka 1987.Makubaliano hayo yanapiga marufuku makombora ya nyuklia ya masafa ya kati.Waziri Rice lakini amesema,Marekani itasonga mbele na mradi wake.