1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Mwaka mmoja tangu kuuwawa mwandishi habari mkosoaji wa Putin

7 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hs

Wanaharakati wa kutetea uhuru leo hii wamepanga kufanya maandamano mjini Moscow Urussi na duniani kote kumshinikiza rais Vladmir Putin kuwasaka waliomuua mwandishi habari Anna Politkovskaya mwaka mmoja uliopita.

Maandamano yatafanyika katika miji mbali mbali ya dunia ikiwa ni pamoja na mjini NewYork,Paris na Roma.

Anna Politkovskaya mwandishi habari aliyekuwa mkosoaji mkubwa war ais Putin aliuwawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya Lifti kwenye nyumba yake mnamo Oktoba saba mwaka jana na hadi sasa hakuna yoyote aliyeshtakiwa kwa mauaji hayo.

Mauaji ya mwandishi huyo wa habari yalikosolewa sana na jumuiya ya kimataifa huku wakosoaji wa Putin wakimshutumu kwa kushindwa kulinda uhuru wa kujieleza.Anna atakumbukwa daima nchini Urussi na duniani kwa jumla kwa kuandika habari bila ya uoga za kuishutumu serikali ya nchi hiyo na maafisa wake wa kijeshi kwa kutumia vibaya madaraka na hasa katika jimbo la mzozo la Chechniya.