1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moyes awataka United kukaza buti

12 Novemba 2013

Kocha wa Manchester United David Moyes ameonya kuwa bado wanapaswa kupiga hatua zaidi baada ya kupata uhai kidogo katika kinyang'anyiro cha kutetea ubingwa wa ligi ya English Premier League

https://p.dw.com/p/1AFvH
Picha: Getty Images

Moyes ameshuhudia timu yake ikipata kipigo dhidi ya Liverpool, mahasimu wao wakubwa Manchester City, na hata West Bromwich Albion tangu mwanzoni mwa msimu, lakini ushindi wa bao 1-0 siku ya Jumamosi wiki hii dhidi ya Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani Old Trafford umeiweka points tano tu nyuma ya Arsenal.

Kipigo dhidi ya Man City na Tottenham Hotspurs mwishoni mwa juma , pamoja na sare ya Chelsea dhidi ya West Bromwich Albion, vimesaidia Manchester United kujiweka miongoni mwa timu zinazowania ubingwa , lakini Moyes amesema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Itachukua muda kidogo kwangu mimi kuweka kila kitu katika mtazamo ninaoutaka. Manuel Pellegrini kocha wa Man City amesema kikosi chake kinapaswa kucheza vizuri zaidi ugenini iwapo kitawania nafasi ya kushinda ubingwa wa Premier League msimu huu. Kikosi cha Pellegrini kina rekodi safi sana nyumbani kikishinda michezo mitano katika ligi hadi sasa msimu huu, lakini ugenini kimevurunda.

Licha ya kupata ushindi hivi karibuni ugenini katika Champions League na kombe la ligi, City wamepata points nne tu katika jumla ya points 18 uginini katika ligi ya Uingereza baada ya kupata kipigo cha nne kwa bao moja bila majibu dhidi ya Sunderland jana Jumapili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / ape /afpe

Mhariri: Mohammed Khelef