1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpanda milima mashuhuri amepewa heshima za mwisho kabla kuzikwa kesho

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvYx

AUCKLAND:

Nchini New Zealand maelfu ya waombolezaji wametoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Edmund Hillary, mtu mashuhuri ambae alijulikana kwa kupanda milima, anaezikwa kesho.Mnamo mwaka wa 1953,Hillary pamoja na wenzake, alikuwa mtu wa kwanza kupanda mlima wa Everest ambao ndio una kilele kirefu kuliko yote dunaini.Kilele hicho kinapatika nchini Nepal.Hillary alifariki mwezi jana akiwa na umri wa miaka 88.Mjini Auckland raia wa Nepal, ndio miongoni mwa watu wa mwanzo kutoa heshima zao. Hillary baada ya kupanda mlima Everest, alitumia mda wake mwingi wa maisha yake kujenga shule na zahanati katika maeneo maskini nchini Nepal.