1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kuwahudumia wakimbizi Uganda wakumbwa na ufisadi

Caro Robi
30 Novemba 2018

Uchunguzi umebaini ufisadi wa mamilioni ya dola na ukosefu wa uwajibikaji katika mpango wa kuwahudumia wakimbizi Uganda.

https://p.dw.com/p/39C2J
Uganda Bürgerkrieg und Hunger im Südsudan treiben Menschen zur Flucht
Picha: Getty Images/D. Kitwood

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wake uliopongwezwa sana  juu ya wakimbizi  nchini Uganda, umegundua ufisadi wa mamilioni ya dola na kutowajibika.

Ripoti ya idara ya ukaguzi wa huduma za ndani ya Umoja huo, umeonesha malipo yalioongezwa hesabu, rushwa na udanganyifu, huku sheria zikikiukwa na kusababisha hasara kwa Shirika linalowahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

Uganda  inawahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni moja ambao wameikimbia Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kutoka nchi nyengine.

Nchi hiyo imekuwa ikipongezwa kwa kuwa sera yake ya kuwafungulia milingo wakimbizi na kuwaruhusu kuwa na uhuru wa kutembea nchini humo, kuweza kupata huduma za afya, pamoja na ardhi ndogo kwa ajili kilimo na makazi.

Shirika hilo la Ukaguzi la Umoja wa Mataifa limechunguza shughuli za Shirika  linalowahudumiwa wakimbizi la Umoja wa Mataifa -UNHCR nchini Uganda  kwa miezi 18 kuanzia Julai 2016.