1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpasuko wa kisiasa kisiwani Zanzibar

14 Agosti 2007

Mpasuko wa kisiasa umechukua sura mpya katika chama cha Civic United Front, CUF. chama hicho kimeanzisha harakati za kuwataka wajumbe wa mataifa ya kigeni waishio nchini humo kuingilia kati suala hilo baada ya mazungumzo kati yao na chama tawala cha CCM kukwama.

https://p.dw.com/p/CH9h
Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa chama cha CUF
Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa chama cha CUFPicha: DW
Kulingana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, mazungumzo hayo ni danadana ndipo wakaamua kutangaza kuwa yamekwama. Viongozi wa vyama vya CUF na CCM walitia saini makubaliano ya kukamilisha mazungumzo hayo ifikapo Agosti 16. CCM kwa upande wake inasisitiza kuwa ndiyo iliyoanzisha mazungumzo hayo na haiwezi kupangwa ratiba. Wakaazi wa Visiwani Zanzibar na Bara wana hisia gani? Thelma Mwadzaya alizungumza na baadhi yao akianza na Zakia Omar.