1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Msichana wa Kitunisia" Blogu iliyopata DW BOBs Award 2011

Mohamed Abdulrahman13 Aprili 2011

Lina Ben Mhenni, msichana kutoka Tunisia, amepata tuzo ya blogu ya kimataifa ya DW BOBs Award.

https://p.dw.com/p/10sHV

Blogu iliopewa jina la  "A Tunisian Girl" (Msichana wa Kitunisia)  imeshinda tuzo ya blogu ya kimataifa ya THE BOBs  inayotolewa na Deutsche Welle-BOB. Tuzo hiyo ilitolewa Aprili 12 mjini Bonn kwa kupitia anuani ya internet  http://atunisiangirl.blogspot.com.

Lina Ben Mhenni mwenye umri wa miaka 27  ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Tunis. Blogu yake hiyo ilihusika pia na ukandamizaji na uchujaji wa habari wakati wa utawala wa rais wa zamani Zein el-Abidinne Ben Ali.

Lina Ben Mhenni Blog Screenshot
Lina Ben Mhenni amepata zawadi ya BOB Awards ya Deutsche WellePicha: Screenshot http://atunisiangirl.blogspot.com/

 Blogu  yake ikatoa mchango wakati wa  vuguvugu la upinzani Desemba  2010 na Januari 2011 katika mji wa Sidi Bouzid na Kasserine na kuripoti kuhusu ukandamizaji wa vyombo vya dola na machafuko. Tangu wakati huo Mhenni anaandika juu ya matatizo yanayoikabili Tunisia kuelekea Demokarasia. Kwa muda mrefu blogu yake ilipigwa marufuku nchini Tunisia, na ikiwezekana tu kusoma yaliomo ikiwa uko nje ya nchi hiyo.

Kutokana na uteuzi huo wiki hii na jopo la kimataifa, tuzo hiyo itatolewa katika fani sita tofauti wakati wa kongamano la Deutsche Welle la vyombo vya habari duniani tarehe 20 Juni mwaka huu 2011 mjini Bonn.