1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtuhumiwa Abrini akiri alivalia kofia mjini Brussels

10 Aprili 2016

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya kigaidi mjini Paris Mohamed Abrini amekiri Jumamosi (09.04.2016) kuwa mtu "aliyevalia kofia" aliyeonekana katika vidio pamoja na watu waliojiripua kwa kujitoa mhanga katika mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/1ISh8
Mohamed Abrini akiwa katika kituo cha kuuzia petroli nchini Ufaransa

Mtuhumiwa wa mashambulizi ya kigaidi mjini Paris Mohamed Abrini amekiri jana Jumamosi (09.04.2016) kuwa mtu "aliyevalia kofia" aliyeonekana katika vidio pamoja na watu waliojiripua kwa kujitoa mhanga katika uwanja wa ndege wa Brussels mwezi uliopita, picha zilizoibua msako mkubwa.

Abrini ameungama katika siku aliyofikishwa mahakamani akishitakiwa kwa mauaji ya kigaidi kuhusiana na mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris ambapo watu 130 waliuwawa, waendesha mashitaka wamesema.

Mtuhumiwa wa ugaidi Osama Krayem , raia wa Sweden , ameshitakiwa pia kwa makosa hayo hayo kuhusiana na jukumu lake katika shambulio la kujitoa muhanga katika kituo cha treni ya mjini mjini Brussels Machi 22, ambalo lilitokea saa moja baada ya mripuko katika uwanja wa ndege. Jumla ya watu 32 walifariki katika mashambulizi hayo yaliyofuatana.

Belgien Brüssel Molenbeek Festnahme Terrorist Salah Abdeslam
Salah Abdeslam wakati akimatwa mjini Brussels Machi mwaka huuPicha: picture-alliance/AP Photo/VTM

Nadharia yathibitika

Kukamatwa huko kwa watu hao kunaimarisha nadharia kwamba kundi hilo la magaidi lilifanya mashambulizi yote mawili ya kigaidi nchini Ufaransa na Ubelgiji , ambayo Dola la Kiislamu lilidai kuhusika.

Watu hao wawili ni miongoni mwa watu sita waliokamatwa katika msako mjini Brussels siku ya Ijumaa. Wawili waliachiwa huru baadaye lakini wawili wengine wameshitakiwa kwa kushiriki kwa madai ya kuwasaidia Abrini na Krayem.

Jaji anayeongoza uchunguzi nchini Ubelgiji kuhusiana na mashambulizi ya mjini Paris Novemba 13 alimfungulia mashitaka Abrini kwa kushiriki katika shughuli za kundi la kigaidi na mauaji ya kigaidi,ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali imesema katika taarifa.

Belgien Maelbeek Metrostation in Brüssel
Kituo cha chini ya ardhi cha Maelbeek mjini BrusselsPicha: Getty Images/C. Furlong

Abrini Mbelgiji mwenye asili ya Morocco alikuwa mtu wa mwisho mshukiwa wa mashambulizi ya mjini Paris. Alionekana katika kamera za CCTV katika kituo cha kuuzia mafuta ya petroli kaskazini ya Paris siku mbili kabla ya mashambulizi mjini humo.

Katika gari pamoja nae alikuwa mshukiwa mwenzake wa shambulizi la mjini Paris Salah Abdeslam, ambaye anasubiri kurejeshwa kutoka Ubelgiji kwenda Ufaransa.

Waendesha mashitaka pia wamethibitisha kuhusika kwa Abrini katika mashambulizi ya uwanja wa ndege wa Brussels.

Abrini mwenye umri wa miaka 31, alikiri kuwapo katika eneo la tukio, wakati alipoonesha ushahidi, ikiwa ni pamoja na video ya mtu asiyetambulika aliyevalia kofia na jaketi la rangi ambayo haukukoza sana akionekana karibu na washambuliaji wa kujitoa muhanga wakati wakitembea katika ukumbi ambao wasafiri husubiri safari wakisukuma toroli lililokuwa na mfuko uliojaa miripuko.

Belgien Place de la Bourse Brüssel
Wakaazi wa mji wa Brussels wakiandika ujumbe katika eneo la tukio la kigaidiPicha: Getty Images/C. Court

Washambuliaji wawili katika uwanja huo wa ndege wametambuliwa kuwa ni El Bakraoui na Najim Laachraoui, wanaoaminika kuwa watengenezaji wa mabomu katika kundi hilo.

Ni mtoto wa mkimbizi

Kaka wa Ibrahim Khalid alijiripua katika kituo cha treni cha chini ya ardhini cha Maalbeek karibu na makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels.

Krayem , mtoto wa mkimbizi kutoka Syria , ametanbuliwa kuwa mtu anayeonekana pamoja na Khalid muda mfupi kabla ya shambulio katika kituo hicho cha treni, wamesema waendesha mashitaka.

Krayem pia alionekana katika kamera akinunua mifuko iliyotumiwa kuvicha mabomu yaliyoripuriwa katika uwanja wa ndege, wameongeza.

Belgien Frankreich Web-Video Foto von Najim Laachraoui alias Soufiane Kayal
Picha ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga Najim LaachraouiPicha: picture-alliance/epa/Belgium Federal Police

Vyombo vya habari vya Sweden vimesema Krayem , mwenye umri wa miaka 23 , ambaye alikulia katika mji wa kusini wa Malmo, na kuchapisha picha za mtu huyo akiwa ameshikilia bunduki ya Kalashnikov mbe ya bendera ya IS ambayo inasemekana ilichukuliwa nchini Syria.

Mtu mmoja aliyekamatwa siku ya Ijumaa na kutambuliwa kuwa ni raia wa Rwanda mwenye umri wa miaka 25 Herve B.M. anatuhumiwa kutoa msaada, kwa Abrini na Krayem, waendesha mashitaka wamesema katika taarifa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Yusra Buwayhid