1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muguruza kumenyana na Azarenka nusu fainali ya Qatar Open

Josephat Charo
5 Machi 2021

Garbine Muguruza wa Uhispania alimpiku Maria Sakkari wa Ugiriki kwa seti mbili za 6-3, 6-1 siku ya Alhamisi na kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya mchezo wa tenisi ya Qatar Open.

https://p.dw.com/p/3qGUP
Tennis, Garbine Muguruza bei Wimbledon
Garbine MuguruzaPicha: picture-alliance/B.Curtis

Muguruza atapambana na Victoria Azarenka wa Belarus, aliyewahi kuwa mchezaji nambari moja wa dunia katika tenisi upande wa wanawake na aliyewahi pia kushinda mashindano mawili makubwa ya mchezo huo.

Muguruza alionyesha kiwango cha juu cha mchezo akimshinikiza mpinzani wake Sakkari ambaye hakuweza kuhimili vishindo vyake. Kwa haraka aliongoza seti ya kwanza kwa 4-0 na hakupoteza mipira aliyoianza yeye, ingawa alikabiliwa na changamoto kidogo katika mchezo wa mwisho wa seti hiyo kabla kupata ushindi.

"Nafurahi, nilijihisi vizuri uwanjani." alisema Muguruza, mshindi wa zamani wa mashindano ya tenisi ya Wimbledon na Roland Garros, baada ya ushindi wake.

"Mpaka sasa nafurahi nimerejea, nikijaribu kukaribia na kukribia fainali," aliongeza

Tennis US Open
Victoria AzarenkaPicha: Reuters/USA Today Sports/D. Parhizkaran

Azarenka, mshindi mara mbili wa mashindano ya tenisi ya Australian Open mwaka 2012 na 2013, alifanikiwa kufuzu kwa nusu fainali kwa kumshinda bingwa wa Ukraine Elina Svitolina kwa seti mbili za 6-2, 6-4.

"Kila mechi ni ngumu, mara zote ni ngumu," aliongeza kusema Muguruza huku akilisubiri pambano lake na Azarenka katika nusu fainali.

Muguruza alimtoa nje ya mashindano ya Qatar Open bingwa mtetezi Aryna Sabalenka siku ya Jumatano kwa seti tatu mfululizo 6-2, 6-7, 6-3.

(afp)