1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharaff anasema wakulaumiwa ni Benazir Bhutto mwenyewe

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl6B

Islamabad:

Rais Pervez Musharaff wa Pakistan amemtwika Benazir Bhuttto sehemu kubwa ya dhamana ya kuuliwa kwake.Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani CBS,rais Musharaff amesema Benazir Bhutto ameyatia mwenyewe maisha yake hatarini,aliposimama wima ndani ya gari yake baada ya kampeni ya uchaguzi huko Rawalpindi.Rais Musharaff anasema serikali yake imefanya kila la kufanya kumlinda Benazir Bhutto.Rais huyo wa Pakistan amesema pengine kifo cha Benazir Bhutto kimesababishwa na risasi iliyompiga kichwani.Chama cha Pakistan People’s Party-PPP kinadai uchunguzi huru ufanyike na kusimamiwa na Umoja wa mataifa.