1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf ajiuzulu

Hamidou18 Agosti 2008

Rais Pervez Musharraf aonelea bora kujiuzulu kabla ya bunge kuamua juu ya hatima yake

https://p.dw.com/p/F098
Picha ya Musharraf yakanyagwa na wapinzani wakePicha: AP


►◄




 Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amejiuzulu hii leo ,mnamo mkesha wa kuanzishwa juhudi za serikali za kutaka kumng'owa madarakani.


Akifikia kilele cha misuko suko iliyomgharimu umaarufu wake,kiongozi huyo wa zamani wa makomando,aliyeingia madarakani katika nchi pekee ya  ya ulimwengu wa kiislam yenye nguvu za kinuklea,october mwaka 1999,kufuatia mapinduzi ambayo hayakumwaga damu,amesalim amri hatimae mbele ya wapinzani wake.


Na pengine kutokana na kupungua tangu hivi karibuni uungaji mkono wa jeshi,na Marekani iliyokua mshirika wake mkubwa katika vita dhidi ya magaidi wa itikadi kali.


Marekani imekua ikizidi kumlauzmu Musharaf kwa kushindwa kupambana ipasavyo na makund8i ya Al Qaida na Taliban waliopiga kambi katika maeneo ya kikabila kaskazini magharibi ya Pakistan.


Akihutubia taifa kwa njia ya televisheni hii leo rais Pervez Musharaff amesema:


Baada ya kutetea ufanisi wa mhula wake wa miaka tisa madarakani na kuutuhuma upande wa upinzani kurtaka kuvuruga misingi ya jamhuri ya kiislam ya Pakistan, Pervez Musharraf amemaliza hotuba yake kwa kusema "hatima yake anawaachia wananchi wa Pakistan."


Serikali ya Pakistan ilitangaza hapo jana azma ya kutaka kutuma maombi bungeni ,ili kumng'owa madarakani jenerali huyo wa zamani,aliyeacha nyadhifa zake za kijeshi kabla ya uchaguzi mkuu mwezi February uliopita.


Washindi wa chaguzi hizo,chama cha PPP cha waziri mkuu wa zamani aliyeuliwa Benazir Bhutto na kile cha kiislam cha Nawaz Shariff,wamepania kumng'owa madarakani Pervez Musharaff wanaemlaumu kwa kuwafukuiza kazi wanasheria waliokosoa  utaratibu wa kuchaguliwa kwake mwaka 2007 na amri ya kutangaza sheria ya hali ya hatari November mwaka jana.


Mbali na hayo,kuna chuki za kibinafsi pia na hasa kutoka waziri mkuu wa zamani Nawaz Shariff.

Hadi dakika ya mwisho Pervez Musharraf hakua akionyesha ishara ya kujiuzulu.


Jana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice alisema  tunanukuu:"halizuki suala la kumpatia kinga ya ukimbizi wa kisiasa Musharraf nchini Marekani pindi aking'olewa madarakani.


Katika miji mikubwa ya Pakistan maelefu ya wananchi wanateremka majiani mara baada ya kusikia habari za kujizulu Musharraf, wakishangiria na kuimba nyimbo dhidi yake.


Musharaff anaondoka katika wakati ambapo Pakistan inakabwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na wimbi la mashambulio ya wafuasi wa itikadi kali yaliyogharimu maisha ya zaidi ya watu 1200 kaqtika kipindi cha mwezi  mmoja uliopita.


Serikali mpya ya Pakistan,ikishinikizwa na Marekani tangu mwezi mmoja uliopita,imeanzisha opereshini kali dhidi ya wafuasi wa al Qaida na Taliban katika maeneo ya kaskazini magharibi ambako Marekani inadai ndiko kunakokutikana ngome za wafuasi wa Al Qaida wanaoongozwa na Ossama Ben laden.