1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muslimbrotherhood yaandamwa Misri

4 Aprili 2008

Mkomoto na kutiwa nguvuni wafuasi wake Muslim Brotherhood ni sehemu ya kero kukizuwia kisishnde uchaguzi wa jumaane.

https://p.dw.com/p/DcCk

Vikosi vya usalama vya Misri, jana kwa mara nyengine, vimewatia mbaroni ,wanachama kadhaa wa upinzani wa chama cha "MUSLIM BROTHERHOOD"-chama cha ndugu wa kiislamu.

Siku 2 kabla ,polisi walitumia mkomoto kupambana na waandamanaji maalfu kadhaa i wa chama hicho.Chama hiki cha kiislamu - cha asili kabisa nchini Misri-kinai

tuhumu serikali ya Misri kuendesha kampeni dhidi yake kabla ya uchaguzi wa mabaraza ya miji wa jumaane hii ijayo.

Bw.Mohammed Habib hatakubali kutishwa kwa kutiwa nguvuni kwa wafuasi kadhaa wa chama chake.

Serikali ya Misri ina azma muda mfupi kabla ya uchaguzi hu kukipiga kumbo kisichaguliwe chama cha Muslim Brotherhood-anadai makamo-rais wa chama.Jaribio hilo lakini, anasema litashindwa kama majaribio kadhaa yaliofanywa hadi sasa.

"Watu wanatimuliwa na kuandamwa.Maandamano hayaruhusiwi wala mikutano ya hadhara ni mwiko.Hairuhusiwi hata kuweka mabiramu.Hatahivyo, tuna njia zetu za kuwasiliana na umma.Tunafanya hivyo kupitia risala yetu kwao:Uislamu ndio suluhisho."

Alisema makamo-rais wa Muslim Brotherhood-Mohammed Habib.

Ni kweli kabisa mkomoto wa vyombo vya usalama nchini Misri una shabaha ya kuzuwia kwa kila hali chama hiki cha upinzani kisishinde.Uchaguzi wa jumaane miongoni mwa mambo mengine unaamua iwapo chama cha Muslim Brotherhood kitaweza katika uchaguzi ujao wa rais kumweka mtetezi wake binafsi.Kufanya hivyo sharti kijipatie madiwani 140 katika uchaguzi huu wa mitaa na ambao wawe kwanza wamechaguliwa.Habib anahofia hawataruhusiwa kufikia idadi hiyo kugombea uchaguzi.

Sio tu chama hiki cha kiislamu kinacholalamika, bali hata mashirika ya haki za binadamu yanakosoa kwa ukali kabisa mkomoto wa vikosi vya usalama vya Misri.

Chama cha HUMAN RIGHTS WATCH kilikwisha lalamika hapo mwishoni mwa mwezi uliopita kukamatwa kwa wafuasi hadi 800 wa chama hicho kabla ya uchaguzi ujao .Chama hicho kimepata dhana kuwa -rais Mubarak anaamini pengine matokeo ya uchaguzi wa jumaane yasiachwe mikononi mwa wapigakra.

Si mara ya kwanza kwa rais Hosni Mubarak kutowaamini wapiga kura wake kuamua.

Rais Mubarak ambae tangu 1981 amekuwa akitawala chini ya msingi wa sheria za hali ya hatari,amekuwa akionekana ni mshirika wa kuaminika wa Marekani na nchi za magharibi katika eneo lenye misukosuko la mashariki ya kati.Lakini kwa jicho la watetezi wa haki za binadamu ambao mwaka baada ya mwaka wakitoa taarifa za kuteswa kwa wafungwa katika magereza ya Misri,Mubarak haonekani kabisa ni mtaywala wa kidemokrasia.Na hata ikiwa angependa sana kutoa sura hiyo hadharani.

Pale katika uchaguzi wa 20005, chama cha ndugu wa kiislamu-Muslim brotherhood hofu za kushinda kwa chama hicho zilipochomoza,rais Hosni Mubarak alijaribu hata kutumia mkono wa chuma kuwazuwia wafuasi wa chama hicho kusogelea vituo vya kupigia kura.

Serikali ya Mubarak inawatilia shaka Muslimbrotherhood kuwa kina ajenda ya kubadili mfumo wa utawala nchini Misri.

Magdi Al Dakkak, muandishi habari na mjumbe wa chama tawala cha rais Mubarak-National democratic party anasema:

"Chama hiki kina mpango unaojulikana wa kuupindua utawala.Kina ajenda ya siri ya kuupindua mfumo wa serikali ya sasa.Muslim Brotherhood kina pia mpango uliodhahiri: kinataka kutoa dhana hadharani kana kwamba ni wademokrasi ambao wana hamu ya kushirikishwa katika shughuli za kisiasa.Jaribio lao kuvaa joho la kidemokrasi na kushiriki katika uchaguzi,ni sehemu ya njama yao ya kisiasa ili kuipindua demokrasia."