1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano kati ya rais Trump na wademocrat unaendelea

Oumilkheir Hamidou
25 Januari 2019

Majadiliano yameanza upya Marekani kati ya wademokrat na warepublican kwa lengo la kusaka ufumbuzi wa muda wa mvutano wa bajeti uliopelekea watumishi wengi wa serikali kulazimika kusalia majumbani mwao au -Shutdown.

https://p.dw.com/p/3CA0x
Shutdown in den USA
Picha: picture-alliance/AA/Y. Ozturk

Mpango uliopendekezwa jana na rais Donald Trump na ule mbadala uliopendekezwa na wademokrat ili kuukwamua mzozo wa bajeti haikusaidia kuungwa mkono vya kutosha katika baraza la seneti.

Kwa zaidi ya mwezi sasa wabunge na rais Trump wanazozana kuhusu mada hiyo hiyo: ukuta ambao rais Trump anataka kuujenga katika mpaka wa Marekani na Mexico ili kukabiliana na wahamiaji kinyume na sheria.

Wakiutaja mpango huo kuwa "hauambatani na maadili" na zaidi kuliko yote "hauna maana," wademocrat wanapinga moja kwa moja kutengwa dala bilioni 5.7 ili kuugharimia. Badala yake wanapendekeza hatua nyengine za ulinzi wa mpakani. Matokeo yake tangu decemba 22 iliyopita watumishi laaki nane wa serikali na watumishi wengine kadhaa wanalazimika kusalia majumbani bila ya malipo.

Spika wa baraza la wawakilishi, Nancy Pelosi
Spika wa baraza la wawakilishi, Nancy PelosiPicha: picture-alliance/AP Photo/J. S. Applewhite

Juhudi za warepublican hazikufaulu

Pendekezo la Republican lililowasilishwa kupigiwa kura kwa mara ya kwanza jana lingesaidia kugharimia shughuli za serikali hadi mwezi wa september na linajumuisha pia fedha za kugharimia ukuta. Repuiblican ndio wanaodhibiti baraza la seneti. Lakini kwa vile wanadhibiti viti 53 kati ya 100, walihitaji kuungwa mkono na wademokrat ili kujipatia sauti 60 zinazohitajika ili pendekezo la rais Trump liweze kufikishwa katika zoezi la mwisho la kupigiwa kura. Hawakufanikiwa kuwatanabahisha wademocrat.

Mara baada ya mapigo yote mawili viongozi wa Republican na Democrat katika baraza la seneti wakakutana kujaribu kuikwamua hali ya mambo.

Ikulu ya Marekani iilidhihirika kuwaachia wasikilizane kuhusu sheria ya kugharimia kwa muda wa wiki tatu kwa masharti kwamba gharama hizo zinajumuisha sehemu kubwa ya fedha za kujenga ukuta.

"Wakiniletea makubaliano ya maana nitayaunga mkono" alisema rais Trump."Bila ya ukuta, hatuwezi kudhamini usalama" amesisitiza mbele ya waandiishi habari.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: picture-alliance/abaca/O. Douliery

Trump amebakiwa na karata moja:sheria ya hali ya hatari

Ufumbuzi wowote unabidi upitie katika baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na Democrarts. Na spika wa baraza hilo, Nancy Pelosi ameshasema hakubaliani na akonti ya kugharimia ukuta."

Bado haijulikani kwa hivyo mzozo utafumbuliwa vipi.

Rais Donald Trump anaonyesha kuwa na njia mbadala za kugharamia ukuta. Ameshawahi hapo awali kuzungumzia uwezekano wa kutangaza sheria ya hali ya hatari ili kukwepa masharti ya bunge.

Kikao kimeakhirishwa hadi baadae leo. Kutokana na kutofikiwa maridhiano rais Trump amelazimika kuakhirisha hotuba yake kwa taifa aliyokuwa aitoe jumanne inayokuja.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP/Reures

Mhariri:Yusuf Saumu