1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja tangu kifo cha Wangari Maathai

25 Septemba 2012

Leo (25.09.2012) ni mwaka mmoja tangu kifo cha mwanamazingira maarufu na mshindi wa tuzo ya Nobeli, Wangari Maathai.

https://p.dw.com/p/16Dgk
Wangari Maathai wakati wa uhai wake
Wangari Maathai wakati wa uhai wakePicha: AP

Msomi huyo anakumbukwa kwa jitihada kubwa katika uhifadhi ya mazingira nchini Kenya ambapo aliunda wakfu uliojulikana kama "Ukanda wa kijani". Katika kuenzi jitihada zake tangu alipofariki Septemba 25 mwaka jana wadau wa mazingira humo wamefanikisha upandaji wa miti zaidi ya milioni 30, matarajio ni kufikia milioni 100 na sasa nguvu zinaelekezwa katika utunzaji wake. Kutoka Nairobi Sudi Mnette alizungumza na Issac Kalua ambae ni mwenyekiti wa wakfu wa Green Africa na kwanza anaelezea anavyomkumbuka Marehemu Wangari Maathai.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed