1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja wa Ebola Kaskazini Mashariki mwa DRC

Angela Mdungu
1 Agosti 2019

Umetimia mwaka mmoja tangu kutangazwa kwa mlipuko wa homa ya Ebola Kaskazini Mashariki mwa Congo. Homa hiyo bado haijadhibitiwa kwa matabibu na hilo linasababisha wakaazi kuishi katika hali isiyo ya kawaida.

https://p.dw.com/p/3N8Vn

UNICEF-Mitarbeiter reinigen sich während einer Schulung zur Infektionsprävention des Ebola-Virus in Juba im Südsudan
Picha: Getty Images/A. Mcbride

Umekuwa mwaka moja wa matatizo katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri, kufuatia mlipuko wa homa ya Ebola katika eneo hilo. Tangu kutangazwa uwepo wa homa ya hiyo katika mikoa ya kaskazini mashariki ya Congo, mfumo wa maisha wa wakaazi umebadilika. Mfano kuosha mikono wakati wowote, kusalimiana bila kumgusa mtu na kadhalika.

Na kile kinachotajwa kuwa kikwazo Katika mpango mzima wakukabiliana na homa ya Ebola katika eneo hili, ni kule kutoelewa kwa wakaazi kwamba Ebola ipo na kuwa inauwa, hasa kufuatia kumgusa mgonjwa au kugusa mwili wa mtu aliefariki kwa homa ya Ebola. Daktari Mwamini Kavugho, aliambukizwa Ebola katika zahanati alikokuwa anafanyia kazi, baada ya kumtibu mtoto mmoja aliyekuwa anaugua Ebola.

Madaktari wafanya kazi kwa tahadhari zaidi

Uwepo wa homa ya Ebola katika mikoa ya Kivu ya kaskazini pamoja na Ituri, umeshawafanya  matabibu katika vituo vya afya kubadili tabia. Awali walikuwa wakiwapokea wagonjwa vizuri, na leo wanawapokea wagonjwa mbalimbali katika hali ya uangalifu, ili kuepukana na maambukizi.

Mmoja wa madaktari, Mayani Chantal anasema awali, wagonjwa mahututi walipokuwa wakiwasili haspitalini hapo walikuwa wakiwapokea kwa haraka na kuwashughulikia lakini kwa sasa wanajizuia kuwagusa wagonjwa kabla ya kujikinga ipasavyo.

Imani ya kuona Ebola inatokomezwa katika eneo hili baada ya Mwaka moja wa mlipuko, inaonekana kupotea, licha ya risala ya profesa Jean-Jacques Muyembe kiongozi wa timu zinazopambana na Ebola, ya kuwa ikiwa raia watasaidiana na timu za matabibu, ebola itatokomezwa katika eneo hili, kwa kipindi cha myezi mitatu au minne. Tangu kuripuka kwa Ebola katika eneo hili, watu zaidi ya elfu moja na mia saba wameshafariki dunia kwa homa hiyo.

Mwandishi: John Kanyunyu DW Beni